Luke 12:53 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baba atakuwa dhidi ya mwanawe, mwana dhidi ya baba yake; mama dhidi ya bintiye, binti dhidi ya mama yake; mamamkwe dhidi ya mke wa mwanawe na huyo dhidi ya mamamkwe wake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watafarakana baba dhidi ya mwanawe na mwana dhidi ya babaye, mama dhidi ya bintiye na binti dhidi ya mamaye, naye mama mkwe dhidi ya mkwewe na mkwe dhidi ya mama mkwe wake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watafarakana baba na mwanawe, na mwana na babaye; mama na binti yake, na binti na mamaye; mkwe mtu na mkwewe, mkwe na mkwe mtu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kina baba watakuwa kinyume cha wana wao: na wana nao watakuwa kinyume cha baba zao. Kina mama watakuwa kinyume cha binti zao: na binti nao watakuwa kinyume cha mama zao. Mama wakwe watakuwa kinyume cha wake za wana wao, na wake za wana wao watakuwa kinyume cha mama wakwe zao.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baba atakuwa dhidi ya mwanawe, mwana dhidi ya baba yake; mama dhidi ya bintiye, binti dhidi ya mama yake; mama mkwe dhidi ya mke wa mwanawe na huyo dhidi ya mama mkwe wake.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baba atakuwa dhidi ya mwanawe, mwana dhidi ya baba yake; mama dhidi ya bintiye, binti dhidi ya mama yake; mamamkwe dhidi ya mke wa mwanawe na huyo dhidi ya mamamkwe wake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watafarakana baba dhidi ya mwanawe na mwana dhidi ya babaye, mama dhidi ya bintiye na binti dhidi ya mamaye, mama mkwe dhidi ya mkwewe. Naye mkwe dhidi ya mama mkwe wake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watafarakana baba dhidi ya mwanawe na mwana dhidi ya babaye, mama dhidi ya bintiye na binti dhidi ya mamaye, naye mama mkwe dhidi ya mkwewe na mkwe dhidi ya mama mkwe wake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watafarakana baba na mwanawe, na mwana na babaye; mama na binti yake, na binti na mamaye; mkwe mtu na mkwewe, mkwe na mkwe mtu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baba atakuwa dhidi ya mwanawe, mwana dhidi ya baba yake; mama dhidi ya bintiye, binti dhidi ya mama yake; mamamkwe dhidi ya mke wa mwanawe na huyo dhidi ya mamamkwe wake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watagombana baba na mwana wake, tena mwana na baba yake, tena mama na mwana wake wa kike, tena mwana wa kike na mama yake, vilevile mkwe na mkwewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watafarakana baba na mwanawe, na mwana na babaye; mama na binti yake, na binti na mamaye; mkwe mtu na mkwewe, mkwe na mkwe mtu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Baba atapingana na mwana wake, na mwana atapingana na baba yake. Mama atapingana na binti yake, na binti atapingana na mama yake. Mama mukwe atapingana na muke wa mutoto wake, na muke yule atapingana na mama mukwe yake.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Baba wa mtu atafarakana na mwanawe, na mwana na baba yake, mama ya mtu na binti yake, na binti na mama yake, mkwe mtu na mkwewe, mkwe na mkwe mtu.