Luke 12:58 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana kama mshtaki wako anakupeleka mahakamani, ingekuwa afadhali kwako kupatana naye mkiwa bado njiani, ili asije akakupeleka mbele ya hakimu, naye hakimu akakutoa kwa polisi, nao wakakutia ndani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ukiwa njiani na mshtaki wako kwenda kwa hakimu, jitahidi kupatana naye mkiwa njiani. La sivyo, atakupeleka kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa afisa, naye afisa atakutupa gerezani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana, unapofuatana na mshitaki wako kwenda kwa mwamuzi, hapo njiani fanya bidii kupatanishwa naye, asije akakuburuta mpaka mbele ya kadhi; yule kadhi akakutia mikononi mwake mwenye kulipiza, na yule mwenye kulipiza akakutupa gerezani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa mtu anakushtaki na ninyi nyote mnaongozana kwenda mahakamani. Jitahidi kadri inavyowezekana kupatana naye mkiwa njiani. Usipopatana naye, atakupeleka kwa hakimu. Na hakimu atakutia hatiani na maofisa wa mahakama watakutupa gerezani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana kama mshtaki wako anakupeleka mahakamani, ingekuwa afadhali kwako kupatana naye mkiwa bado njiani, ili asije akakupeleka mbele ya hakimu, naye hakimu akakutoa kwa polisi, nao wakakutia ndani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana kama mshtaki wako anakupeleka mahakamani, ingekuwa afadhali kwako kupatana naye mkiwa bado njiani, ili asije akakupeleka mbele ya hakimu, naye hakimu akakutoa kwa polisi, nao wakakutia ndani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Uwapo njiani na adui yako kwenda kwa hakimu, jitahidi kupatana naye mkiwa njiani. La sivyo, atakupeleka kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa afisa, naye afisa atakutupa gerezani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Uwapo njiani na mshtaki wako kwenda kwa hakimu, jitahidi kupatana naye mkiwa njiani. La sivyo, atakupeleka kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa afisa, naye afisa atakutupa gerezani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana, unapofuatana na mshitaki wako kwenda kwa mwamuzi, hapo njiani fanya bidii kupatanishwa naye, asije akakuburuta mpaka mbele ya hakimu; yule hakimu akakutia mikononi mwake mwenye kulipiza, na yule mwenye kulipiza akakutupa gerezani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana kama mshtaki wako anakupeleka mahakamani, ingekuwa afadhali kwako kupatana naye mkiwa bado njiani, ili asije akakupeleka mbele ya hakimu, naye hakimu akakutoa kwa polisi, nao wakakutia ndani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mnapokwenda bomani, wewe na mshitaki wako, umkaze njiani, mpatane, maana asikukokote kwa mwenye hukumu, naye mwenye hukumu asikutie mkononi mwa mpiga fimbo, naye mpiga fimbo asikutie kifungoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana, unapofuatana na mshitaki wako kwenda kwa mwamuzi, hapo njiani fanya bidii kupatanishwa naye, asije akakuburuta mpaka mbele ya kadhi; yule kadhi akakutia mikononi mwake mwenye kulipiza, na yule mwenye kulipiza akakutupa gerezani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Unapokwenda kwa tribinali na mupinzani wako, ujikaze upatane naye mungali katika njia. Kama si vile atakupeleka mbele ya mwamuzi, na mwamuzi atakutoa kwa askari, na askari atakutupa katika kifungo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, unapofuatana na mshitaki wako kwenda kwa liwali, njiani ujitahidi kupatanishwa nae: asije akakukokota mbele ya kadhi, yule kadhi akakutia katika mikono ya askari, yule askari akakutupa gerezani.