Luke 12:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Inajulikana kwamba shomoro watano huuzwa kwa sarafu ndogo kumi, au sivyo? Lakini mbele ya Mungu hasahauliki hata mmoja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mnajua kwamba shomoro watano huuzwa kwa senti mbili? Lakini Mungu hamsahau hata mmoja wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Mashomoro watano hawauzwi kwa senti mbili? Wala hasahauliwi hata mmojawapo mbele za Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndege wanapouzwa, ndege watano wadogo wanagharimu senti mbili tu za shaba. Lakini Mungu hasahau hata mmoja wao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Inajulikana kwamba shomoro watano huuzwa kwa senti kumi, au sivyo? Lakini mbele ya Mungu hasahauliki hata mmoja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Inajulikana kwamba shomoro watano huuzwa kwa sarafu ndogo kumi, au sivyo? Lakini mbele ya Mungu hasahauliki hata mmoja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mnajua kwamba shomoro watano huuzwa kwa senti mbili? Lakini Mungu hamsahau hata mmoja wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mnajua kwamba shomoro watano huuzwa kwa senti mbili? Lakini Mungu hamsahau hata mmoja wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Shomoro watano hawauzwi kwa senti mbili? Wala hasahauliwi hata mmojawapo mbele za Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Inajulikana kwamba shomoro watano huuzwa kwa sarafu ndogo kumi, au sivyo? Lakini mbele ya Mungu hasahauliki hata mmoja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Videge vitano haviuzwi kwa senti mbili? Lakini hata mmoja wao hasahauliwi mbele ya Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Mashomoro watano hawauzwi kwa senti mbili? Wala hasahauliwi hata mmojawapo mbele za Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ndege watano wadogo, si wanauzishwa kwa bei chini kabisa? Hata vile Mungu hasahau hata mumoja wao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Haviuzwi videge vitano kwa pesa mbili? na hatta kimojawapo hakisahauliwi mbele ya Mungu: