Luke 12:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Nawaambieni kweli, kila mtu anayekiri hadharani kwamba yeye ni wangu, Mwana wa Mtu naye atakiri mbele ya malaika wa Mungu kwamba mtu huyo ni wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ninawaambia kwamba yeyote atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkiri mbele za malaika wa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nawaambia, kila atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkiri yeye mbele ya malaika wa Mungu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninawaambia, mkinikiri mbele za watu, ndipo nami nitakiri kuwa ninyi ni wangu mbele za Mungu na malaika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Nawaambieni kweli, kila mtu anayekiri hadharani kwamba yeye ni wangu, Mwana wa Mtu naye atakiri mbele ya malaika wa Mungu kwamba mtu huyo ni wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Nawaambieni kweli, kila mtu anayekiri hadharani kwamba yeye ni wangu, Mwana wa Mtu naye atakiri mbele ya malaika wa Mungu kwamba mtu huyo ni wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ninawaambia kwamba, ye yote atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkiri mbele za malaika wa Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ninawaambia kwamba yeyote atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkiri mbele za malaika wa Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nawaambia, kila atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkiri yeye mbele ya malaika wa Mungu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Nawaambieni kweli, kila mtu anayekiri hadharani kwamba yeye ni wangu, Mwana wa Mtu naye atakiri mbele ya malaika wa Mungu kwamba mtu huyo ni wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini nawaambiani: Kila atakayeungama mbele ya watu, kwamba ni mtu wangu, naye Mwana wa mtu ataungama mbele ya malaika wa Mungu, kwamba ni mtu wangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nawaambia, kila atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkiri yeye mbele ya malaika wa Mungu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Nami ninawaambia: kila mutu anayenikubali mbele ya watu, Mwana wa Mutu atamukubali vilevile mbele ya wamalaika wa Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nami nawaambieni, Killa atakaenikiri mbele za watu, Mwana wa Adamu nae atamkiri mbele za malaika wa Mungu.