Luke 13:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo watu fulani walikuja, wakamweleza Yesu juu ya watu wa Galilaya ambao Pilato alikuwa amewaua wakati walipokuwa wanachinja wanyama wao wa tambiko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo huo, kulikuwa na watu waliomwambia Isa habari za Wagalilaya ambao Pilato aliwaua, na damu ya hao watu akaichanganya na dhabihu yao waliyokuwa wanatoa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sehemu ya watu waliokuwa pamoja na Yesu pale, walimweleza kilichowapata baadhi ya waabuduo kutoka Galilaya. Pilato alikuwa ameamuru wauawe. Damu zao zilichanganywa na damu za wanyama waliowaleta kwa ajili ya kutoa dhabihu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakati huo watu fulani walikuja, wakamweleza Yesu juu ya watu wa Galilaya ambao Pilato alikuwa amewaua wakati walipokuwa wanachinja wanyama wao wa tambiko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo watu fulani walikuja, wakamweleza Yesu juu ya watu wa Galilaya ambao Pilato alikuwa amewaua wakati walipokuwa wanachinja wanyama wao wa tambiko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo huo, kulikuwa na watu waliomwambia Yesu habari za Wagalilaya ambao Pilato aliwaua na damu ya hao watu akaichanganya na dhabihu yao waliyokuwa wanatoa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo huo, kulikuwa na watu waliomwambia Isa habari za Wagalilaya ambao Pilato aliwaua, na damu ya hao watu akaichanganya na dhabihu yao waliyokuwa wanatoa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wakati huo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo watu fulani walikuja, wakamweleza Yesu juu ya watu wa Galilaya ambao Pilato alikuwa amewaua wakati walipokuwa wanachinja wanyama wao wa tambiko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Siku zilezile walikuwapo watu waliomsimulia ya Wagalilea, ambao Pilato alimwaga damu zao na kuzichanganya na damu za ng'ombe zao za tambiko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku zile watu wamoja wakakuja kumwelezea Yesu habari juu ya wale watu wa Galilaya waliouawa na liwali Pilato walipokuwa wakichinja nyama za kutolea Mungu sadaka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
WAKATI huohuo walikuwapo watu wakimwarifu khabari za Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao.