Luke 13:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mkuu wa sunagogi alikasirika kwa sababu Yesu alikuwa amemponya huyo mama siku ya Sabato. Hivyo akawaambia wale watu waliokusanyika pale, “Mnazo siku sita za kufanya kazi. Basi, fikeni siku hizo mkaponywe magonjwa yenu; lakini msije siku ya Sabato.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kiongozi wa sinagogi akakasirika kwa sababu Isa alikuwa ameponya mtu siku ya Sabato. Akaambia umati ule wa watu, “Kuna siku sita ambazo watu wanapaswa kufanya kazi. Katika siku hizo, njooni mponywe, lakini si katika siku ya Sabato.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mkuu wa sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akajibu, akawaambia mkutano, Kuna siku sita zifaazo kufanya kazi, basi njoni mponywe katika siku hizo, wala si katika siku ya sabato.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kiongozi wa sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu aliponya siku ya Sabato. Akawaambia watu, “Kuna siku sita za kufanya kazi. Hivyo njooni ili mponywe katika moja ya siku hizo, msije siku ya Sabato kutafuta uponyaji.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini mkuu wa sunagogi alikasirika kwa sababu Yesu alikuwa amemponya siku ya Sabato. Hivyo akawaambia wale watu walikusanyika pale, “Mnazo siku sita za kufanya kazi. Basi, fikeni siku hizo mkaponywe magonjwa yenu; lakini msije siku ya Sabato.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mkuu wa sunagogi alikasirika kwa sababu Yesu alikuwa amemponya huyo mama siku ya Sabato. Hivyo akawaambia wale watu waliokusanyika pale, “Mnazo siku sita za kufanya kazi. Basi, fikeni siku hizo mkaponywe magonjwa yenu; lakini msije siku ya Sabato.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mkuu wa sinagogi, akakasirika kwa sababu Yesu alikuwa ameponya mtu siku ya Sabato. Kwa hiyo mkuu wa sinagogi akaendelea kuuambia ule umati wa watu, “Kuna siku sita ambazo watu wanapaswa kufanya kazi, katika siku hizo, njoni mponywe, lakini si kuja kuponywa siku ya Sabato.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kiongozi wa sinagogi akakasirika kwa sababu Isa alikuwa ameponya mtu siku ya Sabato. Akaambia ule umati wa watu, “Kuna siku sita ambazo watu wanapaswa kufanya kazi. Katika siku hizo, njooni mponywe, lakini si katika siku ya Sabato.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mkuu wa sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akajibu, akawaambia mkutano, Kuna siku sita zifaazo kufanya kazi, basi njoni mponywe katika siku hizo, wala si katika siku ya sabato.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini mkuu wa sunagogi alikasirika kwa sababu Yesu alikuwa amemponya huyo mama siku ya Sabato. Hivyo akawaambia wale watu waliokusanyika pale, “Mnazo siku sita za kufanya kazi. Basi, fikeni siku hizo mkaponywe magonjwa yenu; lakini msije siku ya Sabato.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mkuu wa nyumba ya kuombea akamkasirikia Yesu, kwa sababu amemponya siku ya mapumziko, akawaambia watu waliokuwamo: Ziko siku sita za kufanya kazi; basi, mje siku hizo, mpate kuponywa, lakini msiponywe siku ya mapumziko!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mkuu wa sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akajibu, akawaambia mkutano, Kuna siku sita zifaazo kufanya kazi, basi njoni mponywe katika siku hizo, wala si katika siku ya sabato.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mukubwa wa nyumba ya kuabudia alichukizwa kwa sababu Yesu aliponyesha mutu kwa siku ya Sabato. Kwa hiyo akawaambia watu waliokusanyika pale: “Kuna siku sita za kazi. Basi mufike kwa kuponyeshwa katika siku zile, hapana kwa siku ya Sabato!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mkuu wa ile sunagogi akajibu, akiona hasira kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akawaambia makutano, Kuna siku sita itupasapo kufauya kazi: katika hizo, bassi, njoni mponywe wala si katika siku ya sabato.