Luke 13:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Bwana akamjibu, “Enyi wanafiki! Nani kati yenu hangemfungua ng'ombe wake au punda wake kutoka zizini ampeleke kunywa maji, hata kama siku hiyo ni ya Sabato?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Bwana Isa akamjibu, “Enyi wanafiki! Je, kila mmoja wenu hamfungulii ng’ombe wake au punda wake kutoka zizini akampeleka kumnywesha maji siku ya Sabato?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Bwana akajibu akasema, Enyi wanafiki, kila mmoja wenu, je! Hamfungui ng'ombe wake au punda wake siku ya sabato katika zizi, aende naye kumnywesha?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akamjibu kwa kusema, “Ninyi watu ni wanafiki! Ninyi nyote huwafungulia punda au ng'ombe wenu wa kulimia kutoka zizini na kuwapeleka kunywa maji kila siku, hata siku ya Sabato.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo Bwana akamjibu, “Enyi wanafiki! Nani kati yenu hangemfungua ng'ombe au punda wake kutoka zizini ampeleke kunywa maji, hata kama siku hiyo ni ya Sabato?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Bwana akamjibu, “Enyi wanafiki! Nani kati yenu hangemfungua ng'ombe wake au punda wake kutoka zizini ampeleke kunywa maji, hata kama siku hiyo ni ya Sabato?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Bwana akamjibu, “Enyi wanafiki! Je, kila mmoja wenu hamfungulii ng'ombe wake au punda wake kutoka zizini akampeleka kumnywesha maji siku ya Sabato?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Bwana Isa akamjibu, “Enyi wanafiki! Je, kila mmoja wenu hamfungulii ng’ombe wake au punda wake kutoka zizini akampeleka kumnywesha maji siku ya Sabato?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Bwana akajibu akasema, Enyi wanafiki, kila mmoja wenu, je! Hamfungui ng'ombe wake au punda wake siku ya sabato katika zizi, aende naye kumnywesha?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Bwana akamjibu, “Enyi wanafiki! Nani kati yenu hangemfungua ng'ombe wake au punda wake kutoka zizini ampeleke kunywa maji, hata kama siku hiyo ni ya Sabato?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana akajibu akisema: Enyi wajanja, ninyi nyote hamwafungui ng'ombe au punda wenu zizini siku ya mapumziko na kuwapeleka, wanywe?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Bwana akajibu akasema, Enyi wanafiki, kila mmoja wenu, je! Hamfungui ng’ombe wake au punda wake siku ya sabato katika zizi, aende naye kumnywesha?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Bwana akamujibu: “Ninyi wanafiki! Kuna mutu mumoja kati yenu anayekosa kumufungua ngombe au punda wake toka katika upango kwa siku ya Sabato kwa kumupeleka kunywa maji?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi Bwana akamjibu, akasema, Ewe mnafiki, killa mmoja wenu je! hamfungui ngʼombe wake au punda wake mazizini siku ya sabato, akaenda nae kumnywesha?