Luke 13:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ni kama mbegu ya haradali aliyotwaa mtu mmoja na kuipanda shambani mwake; ikaota na kuwa mti. Ndege wa angani wakajenga viota vyao katika matawi yake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Umefanana na punje ya haradali ambayo mtu aliichukua na kuipanda katika shamba lake. Nayo ikakua, ikawa mti, nao ndege wa angani wakatengeneza viota vyao kwenye matawi yake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Umefanana na punje ya haradali aliyotwaa mtu akaitupa katika shamba lake; ikamea, ikawa mti; ndege wa angani wakakaa katika matawi yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ufalme wa Mungu ni kama mbegu ya haradali. Mtu mmoja aliichukua na kuipanda katika bustani yake. Mbegu ikaota, ikakua na kuwa mti na ndege wakatengeneza viota kwenye matawi yake.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
NI kama mbegu ya haradali aliyotwaa mtu mmoja na kuipanda shambani mwake; ikaota hata ikawa mti. Ndege wa angani wakajenga viota vyao katika matawi yake.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ni kama mbegu ya haradali aliyotwaa mtu mmoja na kuipanda shambani mwake; ikaota na kuwa mti. Ndege wa angani wakajenga viota vyao katika matawi yake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Umefanana na punje ya haradali ambayo ni ndogo sana, ambayo mtu aliichukua na kuipanda katika shamba lake. Nayo ikakua, ikawa mti na ndege wa angani wakatengeneza viota vyao kwenye matawi yake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Umefanana na punje ya haradali ambayo mtu aliichukua na kuipanda katika shamba lake. Nayo ikakua, ikawa mti nao ndege wa angani wakatengeneza viota vyao kwenye matawi yake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Umefanana na punje ya haradali aliyotwaa mtu akaitupa katika shamba lake; ikamea, ikawa mti; ndege wa angani wakakaa katika matawi yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ni kama mbegu ya haradali aliyotwaa mtu mmoja na kuipanda shambani mwake; ikaota na kuwa mti. Ndege wa angani wakajenga viota vyao katika matawi yake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Umefanana na kipunje cha haradali, alichokitwaa mtu na kukitupia shambani kwake. Nacho hukua na kupata kuwa mti, hata ndege wa angani hutua katika matawi yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Umefanana na punje ya haradali aliyotwaa mtu akaitupa katika shamba lake; ikamea, ikawa mti; ndege wa angani wakakaa katika matawi yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Unafanana na mbegu ya haradali mutu mumoja aliyotwaa na kuipanda katika shamba lake. Ikaota na kuwa muti mukubwa, nao ndege wakakuja kujenga chicha zao katikati ya matawi yake.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Umefanana na punje ya kharadali, aliyotwaa mtu akaitupa katika shamba lake, ikakua, ikawa mti mkubwa, ndege za anga wakatua katika matawi yake.