Luke 13:21 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ni kama chachu aliyoitwaa mama mmoja na kuichanganya pamoja na unga madebe mawili na nusu kisha unga wote ukaumuka.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Unafanana na chachu ambayo mwanamke aliichukua akaichanganya katika kiasi kikubwa cha unga hadi wote ukaumuka.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Umefanana na chachu aliyotwaa mwanamke akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachacha wote pia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ufalme wa Mungu unafanana na kiasi kidogo cha chachu ambacho mwanamke hutumia kuchanganya na kilo 20 za unga kutengeneza mkate. Hamira huumua kinyunya chote.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ni kama chachu aliyoitwaa mama mmoja na kuichanganya pamoja na unga debe moja kisha unga wote ukaumuka wote.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ni kama chachu aliyoitwaa mama mmoja na kuichanganya pamoja na unga madebe mawili na nusu kisha unga wote ukaumuka.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Unafanana na chachu ambayo mwanamke aliichukua na kuichanganya kwenye vipimo vitatu vya unga hadi wote ukawa umeumuka.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Unafanana na chachu ambayo mwanamke aliichukua akaichanganya katika kiasi kikubwa cha unga mpaka wote ukaumuka.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Umefanana na chachu aliyotwaa mwanamke akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachacha wote pia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ni kama chachu aliyoitwaa mama mmoja na kuichanganya pamoja na unga madebe mawili na nusu kisha unga wote ukaumuka.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Umefanana na chachu, mwanamke akiitwaa, akaichanganya na pishi tatu za unga, mpaka ukachachwa wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Umefanana na chachu aliyotwaa mwanamke akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachacha wote pia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Unafanana na chachu mwanamuke mumoja aliyoitwaa na kuichanga na vipimo vitatu vya unga kwa kuponda mikate, hata yote ikapata kuvimba.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Umefanana na chachu aliyotwaa mwanamke akaisetiri katika pishi tatu za unga, hatta ukachacha wote pia.