Luke 13:22 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu aliendelea na safari yake kwenda Yerusalemu huku akipitia mijini na vijijini, akihubiri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akapita katika miji na vijiji, akifundisha wakati alisafiri kwenda Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye alikuwa akipita katika miji na vijiji, akifundisha, katika safari yake kwenda Yerusalemu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alikuwa akifundisha katika kila mji na kijiji. Aliendelea kusafiri kuelekea Yerusalemu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alindelea na safari yake kwenda Yerusalemu huku akipitia mijini na vijijini, akihubiri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu aliendelea na safari yake kwenda Yerusalemu huku akipitia mijini na vijijini, akihubiri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akapita katika miji na vijiji akifundisha wakati akisafiri kwenda Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akapita katika miji na vijiji, akifundisha wakati alisafiri kwenda Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye alikuwa akipita katika miji na vijiji, akifundisha, katika safari yake kwenda Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu aliendelea na safari yake kwenda Yerusalemu huku akipitia mijini na vijijini, akihubiri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye alipofanya mwendo wa kwenda Yerusalemu akapita mijini na vijijini akiwafundisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye alikuwa akipita katika miji na vijiji, akifundisha, katika safari yake kwenda Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu alipokuwa katika safari kwenda Yerusalema, alipita katika miji na vijiji akifundisha.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawa akizungukazunguka katika miji ni vijiji, akifundisha, na kufanya safari kwenda Yerusalemi.