Luke 13:25 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati utakuja ambapo mwenye nyumba atainuka na kufunga mlango. Nyinyi mtasimama nje na kuanza kubisha mlango mkisema: ‘Bwana, tufungulie mlango.’ Lakini yeye atawajibu: ‘Sijui mmetoka wapi.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenye nyumba atakapoondoka na kufunga mlango, mtasimama nje mkibisha mlango na kusema, ‘Bwana! Tufungulie mlango!’ “Lakini yeye atawajibu, ‘Siwajui ninyi, wala mtokako.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtu anapoufunga mlango wa nyumba yake, unaweza ukasimama nje na kubisha mlangoni, lakini hataufungua. Mnaweza kusema, ‘Mkuu tufungulie mlango!’ Lakini yeye akawajibu, ‘Siwajui ninyi na mnakotoka sikujui.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Wakati utakuja ambapo mwenye nyumba atainuka na kufunga mlango. Ninyi mtasimama nje na kuanza kupiga hodi mkisema: Bwana, tufungulie mlango. Lakini yeye atawajibu: Sijui mmetoka wapi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati utakuja ambapo mwenye nyumba atainuka na kufunga mlango. Nyinyi mtasimama nje na kuanza kubisha mlango mkisema: ‘Bwana, tufungulie mlango.’ Lakini yeye atawajibu: ‘Sijui mmetoka wapi.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati mwenye nyumba atakapoondoka na kufunga mlango, mtasimama nje mkigonga mlango na kusema, ‘Bwana, utufungulie mlango.’ “Lakini yeye atawajibu, ‘Siwajui ninyi wala mtokako.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati mwenye nyumba atakapoondoka na kufunga mlango, mtasimama nje mkibisha mlango na kusema, ‘Bwana! Tufungulie mlango!’ “Lakini yeye atawajibu, ‘Siwajui ninyi, wala mtokako.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati utakuja ambapo mwenye nyumba atainuka na kufunga mlango. Nyinyi mtasimama nje na kuanza kubisha mlango mkisema: ‘Bwana, tufungulie mlango.’ Lakini yeye atawajibu: ‘Sijui mmetoka wapi.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tangu hapo, mwenye nyumba atakapoinuka na kuufunga mlango, ndipo, mtakapoanza kusimama nje na kuugonga mlango mkisema: Bwana, Bwana, tufungulie! Naye atajibu akiwaambia: Siwajui ninyi, mtokako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mwenye nyumba atakapokwisha kusimama na kufunga mulango, ninyi mutabaki inje na kuanza kupiga hodi na kusema: ‘Bwana, utufungulie.’ Naye atawajibu: ‘Sijui munatokea wapi.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tokea wakati ule atakapoondoka mwenye nyumba na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkinena, Bwana, Bwana! utufungulie; nae akajibu, akawaambieni, Siwajui mtokako;