Luke 13:28 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo kutakuwa na kulia na kusaga meno, wakati mtakapowaona Abrahamu, Isaka na Yakobo na manabii wote wapo katika ufalme wa Mungu, lakini nyinyi wenyewe mmetupwa nje!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ndipo kutakuwako kilio na kusaga meno, mtakapowaona Ibrahimu, Isaka, Yakobo na manabii wote wakiwa katika ufalme wa Mungu, lakini ninyi mkiwa mmetupwa nje.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtamwona Ibrahimu, Isaka, Yakobo na manabii wote wakiwa katika ufalme wa Mungu. Lakini ninyi wenyewe mtatupwa nje. Hapo mtalia na kusaga meno yenu kwa uchungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndipo mtakuwa na kulia na kusaga meno, wakati mtakapowaona Abrahamu, Isaka na Yakobo, na manabii wote wapo katika Ufalme wa Mungu, lakini ninyi wenyewe mmetupwa nje!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo kutakuwa na kulia na kusaga meno, wakati mtakapowaona Abrahamu, Isaka na Yakobo na manabii wote wapo katika ufalme wa Mungu, lakini nyinyi wenyewe mmetupwa nje!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ndipo kutakuwako kilio na kusaga meno, mtakapomwona Abrahamu, Isaki na Yakobo na manabii wote wakiwa katika Ufalme wa Mungu, lakini ninyi mkiwa mmetupwa nje.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ndipo kutakuwako kilio na kusaga meno, mtakapowaona Ibrahimu, Isaka, Yakobo na manabii wote wakiwa katika Ufalme wa Mwenyezi Mungu, lakini ninyi mkiwa mmetupwa nje.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Abrahamu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo kutakuwa na kulia na kusaga meno, wakati mtakapowaona Abrahamu, Isaka na Yakobo na manabii wote wapo katika ufalme wa Mungu, lakini nyinyi wenyewe mmetupwa nje!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndiko, kitakakokuwa kilio na kukereza meno, mtakapowaona akina Aburahamu na Isaka na Yakobo na wafumbuaji wote, wamo katika ufalme wa Mungu, lakini ninyi wenyewe mtajiona, mmetupwa nje.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kule mutalia na kusaga meno, mutakapowaona Abrahamu, Isaka, Yakobo na manabii wote katika Ufalme wa Mungu. Lakini ninyi mutakuwa mumetupwa inje!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hapo kutakuwako kulia na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaak na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, na ninyi wenyewe nikitupwa nje.