Luke 13:29 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu watakuja kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na kusini na kukaa kwenye karamu katika ufalme wa Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu watatoka mashariki na magharibi, kaskazini na kusini, nao wataketi kwenye sehemu walizoandaliwa karamuni katika ufalme wa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watakuja watu toka mashariki na magharibi, na toka kaskazini na kusini, nao wataketi chakulani katika ufalme wa Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu watakuja kutoka mashariki, magharibi, kaskazini na kusini. Watakaa kuizunguka meza ya chakula katika ufalme wa Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu watakuja kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na kusini, watakuja na kukaa kwenye karamu katika Ufalme wa Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu watakuja kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na kusini na kukaa kwenye karamu katika ufalme wa Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu watakuja kutoka mashariki na magharibi, kaskazini na kusini, nao wataketi kwenye sehemu walizoandaliwa karamuni katika Ufalme wa Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu watatoka mashariki na magharibi, kaskazini na kusini, nao wataketi kwenye sehemu walizoandaliwa karamuni katika Ufalme wa Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watakuja watu toka mashariki na magharibi, na toka kaskazini na kusini, nao wataketi chakulani katika ufalme wa Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu watakuja kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na kusini na kukaa kwenye karamu katika ufalme wa Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wako watakaotoka maawioni na machweoni kwa jua na upande wa kaskazini na wa kusini, nao watakaa chakulani katika ufalme wa Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watakuja watu toka mashariki na magharibi, na toka kaskazini na kusini, nao wataketi chakulani katika ufalme wa Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu watakuja toka mashariki na magaribi, kaskazini na kusini, nao wataikaa kula chakula katika Ufalme wa Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na watakuja watu toka maawio ya jua na machweo yake na toka kaskazini na kusini, nao wataketi katika ufalme wa Mungu.