Luke 13:33 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata hivyo, kwa leo, kesho na kesho kutwa, ni lazima niendelee na safari yangu, kwa sababu si sawa nabii auawe nje ya Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sina budi kuendelea na safari yangu leo, kesho na kesho kutwa: kwa maana haiwezekani nabii kufa mahali pengine isipokuwa Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Pamoja na hayo imenipasa kushika njia yangu leo na kesho na kesho kutwa; kwa kuwa haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baada ya hilo, ni lazima niende, kwa sababu manabii wote wanapaswa kufia Yerusalemu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hata hivyo, kwa leo, kesho na kesho kutwa, ni lazima niendelee na safari yangu, kwa sababu si sawa nabii auawe nje ya Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata hivyo, kwa leo, kesho na kesho kutwa, ni lazima niendelee na safari yangu, kwa sababu si sawa nabii auawe nje ya Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sina budi kuendelea na safari yangu leo, kesho na kesho kutwa, kwa maana haiwezekani nabii kufa mahali pengine isipokuwa Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sina budi kuendelea na safari yangu leo, kesho na kesho kutwa: kwa maana haiwezekani nabii kufa mahali pengine isipokuwa Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Pamoja na hayo imenipasa kushika njia yangu leo na kesho na kesho kutwa; kwa kuwa haiwezekani nabii aangamie nje ya Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata hivyo, kwa leo, kesho na kesho kutwa, ni lazima niendelee na safari yangu, kwa sababu si sawa nabii auawe nje ya Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini leo na kesho na kesho kutwa sharti niende, kwani haiwezekani, mfumbuaji auawe, isipokuwa Yerusalemu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Pamoja na hayo imenipasa kushika njia yangu leo na kesho na kesho kutwa; kwa kuwa haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ninapaswa kuendelea na safari yangu leo, kesho na kesho kutwa, kwa sababu haipaswi nabii auawe inje ya Yerusalema.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Illakini imenipasa kushika njia yangu leo na kesho na kesho kutwa, kwa maana haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemi.