Luke 13:34 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Yerusalemu! Ee Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako. Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako pamoja kama kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako pamoja, kama vile kuku akusanyavyo vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga kwa mawe waliotumwa kwako, mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hamkutaka.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yerusalemu! Yerusalemu! Uwauaye manabii. Unawapiga kwa mawe watu waliotumwa na Mungu kwako. Mara ngapi nimetaka kuwasaidia watu wako! Nilitaka kuwakusanya kama kuku anavyovikusanya vifaranga vyake chini ya mbawa zake. Lakini hukuniruhusu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Yerusalemu! We Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako pamoja kama kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, Lakini wewe umekataa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Yerusalemu! Ee Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako. Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako pamoja kama kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ewe Yerusalemu, Yerusalemu, wewe uwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako pamoja kama kuku akusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, lakini hamkutaka!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako pamoja, kama vile kuku akusanyavyo vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga kwa mawe waliotumwa kwako, mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku awakusanyavyo vifaranga wake chini ya mbawa zake, wala hamkutaka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Yerusalemu! Ee Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako. Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako pamoja kama kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yerusalemu, Yerusalemu, unawaua wafumbuaji, ukawapiga mawe waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako, kama kuku anavyovikusanya vifaranga vyake mabawani! Lakini hamkutaka!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga kwa mawe waliotumwa kwako, mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hamkutaka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ewe Yerusalema, Ewe Yerusalema, wewe unayewaua manabii na wajumbe ambao Mungu anakutumia kwa kuwatupia mawe. Mara nyingi nilitaka kuwakusanya wakaaji wako kama vile kuku anavyokusanya vitoto vyake chini ya mabawa yake, lakini ninyi hamukutaka!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ee Yerusalemi, Yerusalemi, uwauae manabii na kuwapiga mawe wao waliotumwa kwako! marra ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hanikutaka!