Luke 13:35 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Haya! Utaachiwa mwenyewe nyumba yako. Basi, nawaambieni, hamtaniona mpaka wakati utakapofika mseme: ‘Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tazama nyumba yenu imeachwa ukiwa. Ninawaambia, hamtaniona tena hadi wakati ule mtakaposema, ‘Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Mwenyezi Mungu.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Angalieni, mmeachiwa nyumba yenu! Nami nawaambia, Hamtaniona tena kamwe, hata mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mungu atakuacha ukiwa. Ninawaambia, hamtaniona tena mpaka wakati ule mtakaposema, ‘Karibu! Mungu ambariki yeye ajaye katika jina la Bwana.’”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Haya, utaachiwa mwenyewe nyumba yako. Naam, hakika nawaambieni, hamtaniona mpaka wakati utakapofika mseme: Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Haya! Utaachiwa mwenyewe nyumba yako. Basi, nawaambieni, hamtaniona mpaka wakati utakapofika mseme: ‘Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tazama nyumba yenu inaachwa ukiwa, ninawaambia hamtaniona tena mpaka wakati ule mtakaposema, ‘Amebarikiwa yeye ajaye katika jina la Bwana.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tazama nyumba yenu imeachwa ukiwa. Ninawaambia, hamtaniona tena mpaka wakati ule mtakaposema, ‘Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Mwenyezi Mungu.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Angalieni, mmeachiwa nyumba yenu! Nami nawaambia, Hamtaniona tena kamwe, hadi mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Haya! Utaachiwa mwenyewe nyumba yako. Basi, nawaambieni, hamtaniona mpaka wakati utakapofika mseme: ‘Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtaona, Nyumba yenu ikiachwa, iwe peke yake! Nawaambiani: Hamtaniona tena mpaka siku ile, mtakaposema: Na atukuzwe ajaye kwa Jina la Bwana!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Angalieni, mmeachiwa nyumba yenu! Nami nawaambia, Hamtaniona tena kamwe, hata mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Makao yenu yataachwa ukiwa. Lakini ninawaambia: tangia sasa hamutaniona tena mpaka mutakaposema: ‘Abarikiwe huyu anayekuja kwa jina la Bwana.’ ”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Angalieni, nyumba yenu imeachwa ukiwa. Amin, nawaambieni, Hamtaniona kabisa hatta wakati ule mtakaposema, Amebarikiwa yeye ajae kwa jina la Bwana.