Luke 13:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Au wale kumi na wanane walioangukiwa na mnara kule Siloamu, wakafa; mnadhani wao walikuwa wakosefu kuliko wengine wote walioishi Yerusalemu?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Au wale watu kumi na wanane waliokufa walipoangukiwa na mnara huko Siloamu: mnadhani wao walikuwa waovu kuliko watu wote walioishi Yerusalemu?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Au wale kumi na wanane, walioangukiwa na mnara huko Siloamu, ukawaua, mwadhani ya kwamba wao walikuwa wakosaji kuliko watu wote waliokaa Yerusalemu?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na vipi kuhusu wale watu kumi na wanane waliokufa pale mnara wa Siloamu ulipowaangukia? Mnadhani walikuwa na dhambi kuliko watu wengine katika mji wa Yerusalemu?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Au wale kumi na wanane walioangukiwa na mnara kule Siloamu wakafa; mnadhani wao walikuwa wakosefu zaidi kuliko wengine wote walioishi Yerusalemu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Au wale kumi na wanane walioangukiwa na mnara kule Siloamu, wakafa; mnadhani wao walikuwa wakosefu kuliko wengine wote walioishi Yerusalemu?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Au wale watu kumi na wanane waliokufa walipoangukiwa na mnara huko Siloamu, mnadhani wao walikuwa waovu kuliko watu wote waliokuwa wanaishi Yerusalemu?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Au wale watu kumi na wanane waliokufa walipoangukiwa na mnara huko Siloamu: mnadhani wao walikuwa waovu kuliko watu wote waliokuwa wanaishi Yerusalemu?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Au wale kumi na wanane, walioangukiwa na mnara huko Siloamu, ukawaua, mwadhani ya kwamba wao walikuwa wakosaji kuliko watu wote waliokaa Yerusalemu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Au wale kumi na wanane walioangukiwa na mnara kule Siloamu, wakafa; mnadhani wao walikuwa wakosefu kuliko wengine wote walioishi Yerusalemu?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Au wale kumi na wanane, uliowaangukia mnara kule Siloa na kuwaua, je? Mwadhani, wamekuwa wenye kulipizwa kuwapita wenyeji wote wa Yerusalemu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Au wale kumi na wanane, walioangukiwa na mnara huko Siloamu, ukawaua, mwadhani ya kwamba wao walikuwa wakosaji kuliko watu wote waliokaa Yerusalemu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile munazani kwamba wale watu kumi na wanane waliokufa munara ulipowaangukia kule Siloamu, walikuwa wakosaji kuliko wakaaji wengine wote wa Yerusalema?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Au wale kumi na wanane walioangukiwa na mnara katika Siloam, ukawaangamiza, mwadhani ya kuwa walikuwa wakosaji kuliko watu wote wakaao Yerusalemi?