Luke 13:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Yesu akawaambia mfano huu: “Mtu mmoja alikuwa na mtini shambani mwake. Mtu huyu akaenda akitaka kuchuma matunda yake, lakini akaukuta haujazaa hata tunda moja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Isa akawaambia mfano huu: “Mtu mmoja alikuwa na mtini uliopandwa katika shamba lake la mizabibu, akaja ili kutafuta tini kwenye mti huo, lakini hakupata hata moja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akawasimulia mfano huu: “Mtu mmoja alikuwa amepanda mtini katika shamba lake. Alipokuja kutafuta matunda kwenye mtini huo hakupata tunda lolote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha, Yesu akawaambia mfano huu: “Mtu mmoja alikuwa na mtini katika shamba lake. Mtu huyu akaenda akitaka kuchuma matunda yake, lakini akaukuta haujazaa hata tunda moja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Yesu akawaambia mfano huu: “Mtu mmoja alikuwa na mtini shambani mwake. Mtu huyu akaenda akitaka kuchuma matunda yake, lakini akaukuta haujazaa hata tunda moja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Yesu akawaambia mfano huu: “Mtu mmoja alikuwa na mtini uliopandwa katika shamba lake la mizabibu, akaja ili kutafuta tini kwenye mti huo, lakini hakupata hata moja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Isa akawaambia mfano huu: “Mtu mmoja alikuwa na mtini uliopandwa katika shamba lake la mizabibu, akaja ili kutafuta tini kwenye mti huo, lakini hakupata hata moja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Yesu akawaambia mfano huu: “Mtu mmoja alikuwa na mtini shambani mwake. Mtu huyu akaenda akitaka kuchuma matunda yake, lakini akaukuta haujazaa hata tunda moja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akausema mfano huu: Mtu alikuwa na mkuyu uliopandwa mizabibuni kwake. Alipokuja kutafuta matunda yake hakuyaona.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Yesu akawaambia mufano huu: “Mutu mumoja alikuwa na muti wa tini uliopandwa katika shamba lake la mizabibu. Alikuja kutafuta matunda juu yake, lakini hakupata kitu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akanena mfano huu: Mtu mmoja alikuwa na mtini, umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake wala hakupata.