Luke 13:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, akamwambia mfanyakazi wake: ‘Angalia! Kwa miaka mitatu nimekuwa nikija kuchuma matunda ya mtini huu, bila kupata chochote. Ukate! Kwa nini uitumie ardhi bure?’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo akamwambia mtunza shamba: ‘Tazama, kwa muda wa miaka mitatu sasa nimekuwa nikija kutafuta matunda kwenye mtini huu, nami sikupata hata moja. Ukate! Kwa nini uendelee kuharibu ardhi?’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alikuwa na mtumishi aliyekuwa akilitunza shamba. Hivyo alimwambia mtumishi wake, ‘Nimekuwa nikitafuta matunda kwenye mti huu kwa miaka mitatu, lakini sijawahi kupata tunda lolote. Ukate mti huu! Kwa maana unaiharibu ardhi.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, akamwambia mfanyakazi wake: Angalia! Kwa miaka mitatu nimekuwa nikija kuchuma matunda ya mtini huu, nami nisiambulie kitu. Ukate! Kwa nini uitumie ardhi bure?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, akamwambia mfanyakazi wake: ‘Angalia! Kwa miaka mitatu nimekuwa nikija kuchuma matunda ya mtini huu, bila kupata chochote. Ukate! Kwa nini uitumie ardhi bure?’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo akamwambia mtunza shamba: ‘Tazama, kwa muda wa miaka mitatu sasa nimekuwa nikija kutafuta matunda kwenye mtini huu, nami sikupata hata moja. Ukate! Kwa nini uendelee kuharibu ardhi?’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo akamwambia mtunza shamba: ‘Tazama, kwa muda wa miaka mitatu sasa nimekuwa nikija kutafuta matunda kwenye mtini huu, nami sikupata hata moja. Ukate! Kwa nini uendelee kuharibu ardhi?’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii nimekuja kutafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, akamwambia mfanyakazi wake: ‘Angalia! Kwa miaka mitatu nimekuwa nikija kuchuma matunda ya mtini huu, bila kupata chochote. Ukate! Kwa nini uitumie ardhi bure?’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akamwambia mlimia mizabibu: Tazama, imepita miaka mitatu, tangu nilipoanza kuja kutafuta matunda ya mkuyu huu, lakini siyaoni. Basi, uukate! Hulizuiliani shamba?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi akamwambia mutunzaji wa hili shamba: ‘Sasa ni muda wa miaka mitatu ninakuja kutafuta matunda juu ya muti huu wa tini nami sipati kitu. Uukate! Muti huu unaharibu udongo bure.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda katika mtini huu, nisipate. Ukate, kwa nini uiharibu inchi pia?