Luke 14:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku moja ya Sabato, Yesu alikwenda kula chakula nyumbani kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo, na watu waliokuwapo hapo wakawa wanamchunguza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku moja ya Sabato, Isa alipoenda kula chakula kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo, watu walikuwa wakimchunguza kwa makini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa alipoingia ndani ya nyumba ya mtu mmoja miongoni mwa wakuu wa Mafarisayo siku ya sabato, ale chakula, walikuwa wakimvizia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Siku moja ya Sabato Yesu alikwenda nyumbani kwa miongoni mwa viongozi wa Mafarisayo kula chakula pamoja naye. Watu wote mahali pale walikuwa wanamwangalia kwa makini kuona atafanya nini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Siku moja ya Sabato, Yesu alikwenda kula chakula nyumbani kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo; watu waliokuwapo hapo wakawa wanamchunguza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku moja ya Sabato, Yesu alikwenda kula chakula nyumbani kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo, na watu waliokuwapo hapo wakawa wanamchunguza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikawa siku moja Yesu alipokuwa amekwenda kula chakula kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo siku ya Sabato, watu walikuwa wakimchunguza kwa bidii.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikawa siku moja Isa alipokuwa amekwenda kula chakula kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo siku ya Sabato, watu walikuwa wakimchunguza kwa bidii.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa alipoingia ndani ya nyumba ya mtu mmoja miongoni mwa wakuu wa Mafarisayo siku ya sabato, ale chakula, walikuwa wakimvizia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku moja ya Sabato, Yesu alikwenda kula chakula nyumbani kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo, na watu waliokuwapo hapo wakawa wanamchunguza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Ikawa, alipoingia siku ya mapumziko nyumbani mwa mkuu wa Mafariseo, ale chakula, wakawa wakimtunduia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa alipoingia ndani ya nyumba ya mtu mmoja miongoni mwa wakuu wa Mafarisayo siku ya sabato, ale chakula, walikuwa wakimvizia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja ya Sabato, Yesu aliingia katika nyumba ya mumoja wa wakubwa wa Wafarisayo kwa kula chakula. Mule watu wakabaki wakimuchunguza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
IKAWA, Yesu alipoingia katika nyumba ya mtu mmoja, mtu mkuu katika Mafarisayo, siku ya sabato, ale chakula, walikuwa wakimvizia.