Luke 14:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mmoja wa wale waliokuwa wameketi pamoja na Yesu akasema, “Ana heri mtu yule atakayekula chakula katika ufalme wa Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mmoja wa wale waliokuwa pamoja naye mezani aliposikia hivi akamwambia Isa, “Amebarikiwa mtu yule atakayekula katika karamu ya ufalme wa Mungu!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi aliposikia hayo mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye alimwambia, Heri yule atakayekula mkate katika ufalme wa Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Basi mmoja wa watu waliokuwa mezani pamoja naye aliposikia hayo akamwambia Yesu, “Wamebarikiwa watakaokula karamu katika ufalme wa Mungu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mmoja wa wale waliokuwa wameketi pamoja na Yesu akasema, “Ana heri mtu yule atakayekula chakula katika Ufalme wa Mungu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mmoja wa wale waliokuwa wameketi pamoja na Yesu akasema, “Ana heri mtu yule atakayekula chakula katika ufalme wa Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mmoja wa wale waliokuwa pamoja naye mezani aliposikia hivi akamwambia Yesu, “Amebarikiwa mtu yule atakayekula katika karamu ya Ufalme wa Mungu!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mmoja wa wale waliokuwa pamoja naye mezani aliposikia hivi akamwambia Isa, “Amebarikiwa mtu yule atakayekula katika karamu ya Ufalme wa Mwenyezi Mungu!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi aliposikia hayo mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye alimwambia, Heri yule atakayekula mkate katika ufalme wa Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mmoja wa wale waliokuwa wameketi pamoja na Yesu akasema, “Ana heri mtu yule atakayekula chakula katika ufalme wa Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mmoja wao walikaa pamoja naye chakulani alipoyasikia haya akamwambia: Mwenye shangwe ndiye atakayekula chakula katika ufalme wa Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi aliposikia hayo mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye alimwambia, Heri yule atakayekula mkate katika ufalme wa Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu mumoja kati ya wale waliokuwa wakiikaa kula pamoja na Yesu aliposikia maneno hayo, akamwambia: “Heri mutu atakayeshiriki kwa kula karamu katika Ufalme wa Mungu!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi mtu mmoja katika hawo walioketi pamoja nae, alipoyasikia haya, akamwambia, Yu kheri atakaekula mkate katika ufalme wa Mungu.