Luke 14:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wote, mmoja baada ya mwingine, wakaanza kuomba radhi. Wa kwanza akamwambia mtumishi: ‘Nimenunua shamba, na hivyo sina budi niende kuliangalia; nakuomba uniwie radhi.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Lakini wote, kila mmoja, wakaanza kutoa udhuru: Wa kwanza akasema, ‘Nimenunua shamba, lazima niende kuliona. Tafadhali niwie radhi.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini wageni waalikwa wote walisema kuwa hawawezi kuja. Kila mmoja alitoa udhuru. Wa kwanza alisema, ‘Nimenunua shamba, hivyo ni lazima niende nikalitazame. Tafadhali unisamehe.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini wote, kwa namna moja, wakaanza kuomba radhi. Wa kwanza akamwambia mtumishi: Nimenunua shamba, kwa hiyo sina budi kwenda kuliangalia; nakuomba uniwie radhi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wote, mmoja baada ya mwingine, wakaanza kuomba radhi. Wa kwanza akamwambia mtumishi: ‘Nimenunua shamba, na hivyo sina budi niende kuliangalia; nakuomba uniwie radhi.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Lakini wote, kila mmoja, wakaanza kutoa udhuru: Wa kwanza akasema, ‘Nimenunua shamba, lazima niende kuliona. Tafadhali niwie radhi.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Lakini wote, kila mmoja, wakaanza kutoa udhuru: Wa kwanza akasema, ‘Nimenunua shamba, lazima niende kuliona. Tafadhali niwie radhi.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wote, mmoja baada ya mwingine, wakaanza kuomba radhi. Wa kwanza akamwambia mtumishi: ‘Nimenunua shamba, na hivyo sina budi niende kuliangalia; nakuomba uniwie radhi.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaanza wote pamoja kuja kujipuzapuza. Wa kwanza akamwambia: Nimenunua shamba, sina budi kwenda, nilitazame; nakuomba, usiniwekee mfundo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wao wote moja kwa moja wakaanza kutoa sababu zao za kutokufika. Wa kwanza akamwambia yule mutumishi: ‘Nimenunua shamba, nami ninapaswa kwenda kuliangalia. Tafazali, unisamehe.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakaanza kutoa udhuru, wote pia kwa nia moja. Wa kwanza akamwambia, Nimenunua shamba, sina buddi kwenda na kulitazama; nakuomba, unisamehe.