Luke 14:21 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtumishi huyo akarudi na kumwarifu bwana wake jambo hilo. Yule mwenye nyumba alikasirika, akamwambia mtumishi wake: ‘Nenda upesi kwenye barabara na vichochoro vya mji, uwalete hapa ndani maskini, viwete, vipofu na vilema wengine.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Yule mtumishi akarudi, akampa bwana wake taarifa. Ndipo yule mwenye nyumba akakasirika, akamwagiza yule mtumishi wake, akisema, ‘Nenda upesi kwenye mitaa na vichochoro vya mjini uwalete maskini, vilema, vipofu na viwete.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo mtumishi alirudi na kumjulisha bwana kilichotokea. Bwana wake akakasirika, akamwambia mtumishi wake, ‘Fanya haraka! Nenda mitaani na katika vichochoro vya mji. Niletee maskini, vilema, wasiyeona na walemavu wa miguu!’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mtumishi huyo akarudi na kumwarifu bwana wake jambo hilo. Yule mwenye nyumba alikasirika, akamwambia mtumishi wake: Nenda upesi kwenye barabara na vichochoro vya mji, uwalete hapa ndani maskini, viwete, vipofu na waliolemaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtumishi huyo akarudi na kumwarifu bwana wake jambo hilo. Yule mwenye nyumba alikasirika, akamwambia mtumishi wake: ‘Nenda upesi kwenye barabara na vichochoro vya mji, uwalete hapa ndani maskini, viwete, vipofu na vilema wengine.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Yule mtumishi akarudi, akampa bwana wake taarifa. Ndipo yule mwenye nyumba akakasirika, akamwagiza yule mtumishi wake akisema, ‘Nenda upesi kwenye mitaa na vichochoro vya mjini uwalete maskini, vilema, vipofu na viwete.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Yule mtumishi akarudi, akampa bwana wake taarifa. Ndipo yule mwenye nyumba akakasirika, akamwagiza yule mtumishi wake, akisema, ‘Nenda upesi kwenye mitaa na vichochoro vya mjini uwalete maskini, vilema, vipofu na viwete.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yule mtumwa akaenda, akamwambia Bwana wake kuhusu mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtumishi huyo akarudi na kumwarifu bwana wake jambo hilo. Yule mwenye nyumba alikasirika, akamwambia mtumishi wake: ‘Nenda upesi kwenye barabara na vichochoro vya mji, uwalete hapa ndani maskini, viwete, vipofu na vilema wengine.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, mtumwa akarudi, akamsimulia bwana wake. Ndipo, yule mwenye nyumba alipochafuka, akamwambia mtumwa wake: Toka, uende upesi, ufike kwenye viwanja na njia za mjini, ulete wakiwa na wavilema na vipofu na viwete, uwaingize humu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi yule mutumishi akarudia na kumwelezea bwana wake maneno hayo yote. Halafu bwana wa nyumba akakasirika, na kumwambia: ‘Kwenda upesi katika nafasi za mukutano na katika barabara za muji, uwalete wamasikini, vilema, vipofu na viwete na kuwaingiza humu.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yule mtumishi akaenda, akamwarifu Bwana wake mambo haya. Ndipo yule mwenye nyumba akaghadhabika, akamwambia mtumishi wake, Toka upesi ukaende njia kuu na vichochoro vya mji, ukalete hapa maskini, na vilema, na viwete, na vipofu.