Luke 14:26 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mtu yeyote akija kwangu, asipomchukia baba yake, mama yake, mke wake, watoto, ndugu na dada zake, naam, hata na nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mtu yeyote anayekuja kwangu hawezi kuwa mwanafunzi wangu kama hatanipenda mimi zaidi ya baba yake na mama yake, mke wake na watoto wake, ndugu zake na dada zake, naam, hata maisha yake mwenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Ikiwa unakuja kwangu na hauko tayari kuiacha familia yako, huwezi kuwa mfuasi wangu. Ukimpenda zaidi baba yako, mama yako, mke wako, watoto wako, kaka na dada zako na hata maisha yako zaidi yangu huwezi kuwa mwanafunzi wangu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Mtu yeyote akija kwangu, asipowachukia baba na mama yake, mke wake, watoto, ndugu na dada zake, naam, hata na nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mtu yeyote akija kwangu, asipomchukia baba yake, mama yake, mke wake, watoto, ndugu na dada zake, naam, hata na nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mtu ye yote anayekuja kwangu hawezi kuwa mwanafunzi wangu kama hatanipenda mimi zaidi ya baba yake na mama yake, mke wake na watoto, ndugu zake na dada zake, naam, hata maisha yake mwenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mtu yeyote anayekuja kwangu hawezi kuwa mwanafunzi wangu kama hatanipenda mimi zaidi ya baba yake na mama yake, mke wake na watoto wake, ndugu zake na dada zake, naam, hata maisha yake mwenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake wa kiume na wa kike; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mtu yeyote akija kwangu, asipomchukia baba yake, mama yake, mke wake, watoto, ndugu na dada zake, naam, hata na nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu akija kwangu asipomchukia baba yake na mama yake na mkewe na watoto wake na ndugu zake wa kiume na wa kike, hata asipoichukia roho yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mutu anayenifuata, atakuwa kweli mwanafunzi wangu kama akinipendelea mimi kuliko baba na mama yake, muke na watoto wake, wakaka na wadada zake. Na zaidi ya hii hapaswi kujipendelea yeye mwenyewe vilevile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mtu akija kwangu, nae hamehukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake wanaume na wanawake, na uzima wake pia, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.