Luke 14:28 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa maana, ni nani miongoni mwenu ambaye akitaka kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama zake ili ajue kama ana kiasi cha kutosha cha kumalizia?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ni nani miongoni mwenu ambaye kama anataka kujenga nyumba, hakai kwanza chini na kufanya makisio ya gharama aone kama ana fedha za kutosha kukamilisha?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa unataka kujenga nyumba, kwanza utakaa na kuamua ili kujua itakugharimu kiasi gani. Ni lazima uone ikiwa una pesa za kutosha kumaliza kazi ya ujenzi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa maana, ni nani miongoni mwenu ambaye akitaka kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama zake ili ajue kama ana kiasi cha kutosha cha kumalizia?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa maana, ni nani miongoni mwenu ambaye akitaka kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama zake ili ajue kama ana kiasi cha kutosha cha kumalizia?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ni nani miongoni mwenu ambaye kama anataka kujenga nyumba, hakai kwanza chini na kufanya makisio ya gharama aone kama ana fedha za kutosha kukamilisha?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ni nani miongoni mwenu ambaye kama anataka kujenga nyumba, hakai kwanza chini na kufanya makisio ya gharama aone kama ana fedha za kutosha kukamilisha?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, haketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa maana, ni nani miongoni mwenu ambaye akitaka kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama zake ili ajue kama ana kiasi cha kutosha cha kumalizia?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maana kwenu yuko mtu anayetaka kujenga mnara, asiyekaa kwanza na kuzihesabu shilingi za jengo, kama anazo za kulitimiza?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni nani kati yenu anayetaka kujenga munara, atakayekosa kwanza kuikaa na kuhesabu mali yote atakayoitumia kwa kujenga kusudi ajue kama yuko na mali inayotosha kwa kumaliza?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuihesabu gharama kama ana vitu vya kuumaliza?