Luke 14:31 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Au, ni mfalme gani ambaye akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, hataketi kwanza na kufikiri kama ataweza, kwa askari wake10,000, kumkabili yule aliye na askari 20,000?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Au je, mfalme fulani akienda vita na mfalme mwingine, si yeye huketi chini kwanza na kufikiri: je, akiwa na jeshi la watu elfu kumi, ataweza kupigana na yule anayekuja na jeshi la watu elfu ishirini?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa mfalme anakwenda kupigana vita na mfalme mwingine, atakaa chini kwanza na kupanga. Ikiwa ana askari elfu kumi, ataamua ikiwa ana uwezo wa kumshinda mfalme mwenye askari elfu ishirini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Au, ni mfalme gani ambaye, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, hataketi kwanza chini na kufikiri kama ataweza, kwa askari wake elfu ishirini?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Au, ni mfalme gani ambaye akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, hataketi kwanza na kufikiri kama ataweza, kwa askari wake10,000, kumkabili yule aliye na askari 20,000?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Au ni mfalme gani atokaye kwenda kupigana vita na mfalme mwingine, ambaye hakai chini kwanza na kufikiri iwapo akiwa na jeshi la watu 10,000 ataweza kupigana na yule anayekuja na jeshi la watu 20,000?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Au ni mfalme gani atokaye kwenda kupigana vita na mfalme mwingine, ambaye hakai chini kwanza na kufikiri iwapo akiwa na jeshi la watu 10,000 ataweza kupigana na yule anayekuja na jeshi la watu 20,000?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, haketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Au, ni mfalme gani ambaye akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, hataketi kwanza na kufikiri kama ataweza, kwa askari wake10,000, kumkabili yule aliye na askari 20,000?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Au yuko mfalme anayekwenda vitani kushindana na mfalme mwenzake pasipo kukaa kwanza na kufikiri, kama ataweza kuwatuma askari wake elfu kumi, wakutane na yule anayemjia na askari elfu ishirini?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Au ni mufalme gani anayetaka kwenda kupigana vita na mufalme mwingine, atakayekosa kwanza kuikaa na kujiuliza kama kwa nguvu za waaskari wake elfu kumi ataweza kumushinda adui yake anayekuja na waaskari elfu makumi mbili?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Au mfalme gani, kama anakwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana nae anaemjia pamoja na watu elfu ishirini?