Luke 14:32 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama anaona hataweza, atawatuma wajumbe kutaka masharti ya amani wakati mfalme huyo mwingine angali mbali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikiwa hawezi, basi yule mwingine akiwa bado yuko mbali, yeye hutuma wajumbe na kuomba masharti ya amani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akali mbali.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Akiona hawezi kumshinda mfalme mwingine, atatuma baadhi ya watu kwa mfalme mwingine ili wapatane akiwa bado yuko mbali.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama anaona hataweza, atawatuma wajumbe kutaka masharti ya amani wakati mfalme huyo mwingine angali mbali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama anaona hataweza, atawatuma wajumbe kutaka masharti ya amani wakati mfalme huyo mwingine angali mbali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama hawezi, basi wakati yule mwingine akiwa bado yuko mbali, yeye hutuma ujumbe wa watu na kuomba masharti ya amani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama hawezi, basi wakati yule mwingine akiwa bado yuko mbali, yeye hutuma ujumbe wa watu na kuomba masharti ya amani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akiwa bado mbali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama anaona hataweza, atawatuma wajumbe kutaka masharti ya amani wakati mfalme huyo mwingine angali mbali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama haviwezi, atatuma wajumbe, yule mwingine akingali mbali bado, amwombe mapatano.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akali mbali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeye akiona kwamba hataweza, atamutumia yule mufalme mwingine ujumbe kwa kuomba mapatano ya amani, huyo mwingine anapokuwa angali mbali.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kama sivyo, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, yule mtu akiwa angali mbali.