Luke 14:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu akawaambia, “Ni nani kati yenu ambaye mtoto wake au ng'ombe wake akitumbukia shimoni, hangemtoa hata kama ni siku ya Sabato?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akawauliza, “Kama mmoja wenu angekuwa na mtoto au ng’ombe wake aliyetumbukia katika kisima siku ya Sabato, je, hamtamvuta mara moja na kumtoa?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia, Ni nani miongoni mwenu, ikiwa ng'ombe wake au punda wake ametumbukia kisimani, asiyemwopoa mara hiyo siku ya sabato?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha akawaambia Mafarisayo na wanasheria, “Ikiwa mwanao au mnyama wako atatumbukia kisimani siku ya Sabato, mnatambua kuwa mtamtoa haraka.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Halafu akawaambia, “Ni nani kati yenu ambaye mtoto wake au ng'ombe wake akitumbukia shimoni, hangemtoa hata kama ni siku ya Sabato?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu akawaambia, “Ni nani kati yenu ambaye mtoto wake au ng'ombe wake akitumbukia shimoni, hangemtoa hata kama ni siku ya Sabato?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akawauliza, “Kama mmoja wenu angekuwa na mtoto au ng'ombe wake aliyetumbukia katika kisima siku ya Sabato, je, hamtamvuta mara moja na kumtoa?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akawauliza, “Kama mmoja wenu angekuwa na mtoto au ng’ombe wake aliyetumbukia katika kisima siku ya Sabato, je, hamtamvuta mara moja na kumtoa?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia, Ni nani miongoni mwenu, ikiwa ng'ombe wake au punda wake ametumbukia kisimani, asiyemwopoa mara hiyo siku ya sabato?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu akawaambia, “Ni nani kati yenu ambaye mtoto wake au ng'ombe wake akitumbukia shimoni, hangemtoa hata kama ni siku ya Sabato?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akawaambia wale: Kwenu yuko mwenye punda au ng'ombe asiyemwopoa papo hapo, akitumbukia kisimani, hata ikiwa siku ya mapumziko?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia, Ni nani miongoni mwenu, ikiwa ng’ombe wake au punda wake ametumbukia kisimani, asiyemwopoa mara hiyo siku ya sabato?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akawaambia wale watu: “Ni nani kati yenu mutoto wake au ngombe wake akitumbukia ndani ya kisima, atakayekosa mara moja kumwondosha mule hata ikiwa ni siku ya Sabato?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akajibu akawaambia, Nani wenu mwenye punda au ngʼombe ametumbukia kisimani, asiyemwondoa marra moja siku ya sabato?