Luke 15:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alipoanza kupata akili, akafikiri: ‘Mbona kuna wafanyakazi wengi wa baba yangu wanaokula na kusaza, nami ninakufa njaa?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Lakini alipozingatia moyoni mwake, akasema, ‘Ni watumishi wangapi walioajiriwa na baba yangu ambao wana chakula cha kuwatosha na kusaza, bali mimi hapa nakufa kwa njaa!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alipotambua namna alivyokuwa mjinga, akafikiri moyoni mwake na kusema, ‘Wafanyakazi wote wa baba yangu wana chakula kingi. Lakini niko hapa kama niliyekufa kwa sababu sina chakula.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alipoanza kupata akili akafikiri: Mbona kuna wafanyakazi wengi wa baba yangu wanaokula na kusaza, nami ninakufa njaa?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alipoanza kupata akili, akafikiri: ‘Mbona kuna wafanyakazi wengi wa baba yangu wanaokula na kusaza, nami ninakufa njaa?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Lakini alipozingatia moyoni mwake, akasema, ‘Ni watumishi wangapi walioajiriwa na baba yangu ambao wana chakula cha kuwatosha na kusaza, bali mimi hapa nakufa kwa njaa!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Lakini alipozingatia moyoni mwake, akasema, ‘Ni watumishi wangapi walioajiriwa na baba yangu ambao wana chakula cha kuwatosha na kusaza, bali mimi hapa nakufa kwa njaa!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kubakiza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alipoanza kupata akili, akafikiri: ‘Mbona kuna wafanyakazi wengi wa baba yangu wanaokula na kusaza, nami ninakufa njaa?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, alipojirudia mwenyewe akisema: Vibarua wangapi wako kwa baba yangu wanaoshiba chakula na kusaza, nami hapa ninakufa njaa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi akaanza kufikiri yeye mwenyewe na kujisemesha: ‘Watumishi wote wa baba yangu wana vyakula kwa uwingi, nami huku ninakufa na njaa!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta alipojirudia nafsi yake, akasema, Watumishi wa mshahara wangapi wa baba yangu wanakula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa.