Luke 15:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, akaanza safari ya kurudi kwa baba yake. Alipokuwa bado yu mbali, baba yake alimwona, na kwa moyo wa huruma alimkimbilia, akamkumbatia na kumbusu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi akaondoka, akaenda kwa baba yake. “Lakini alipokuwa bado yuko mbali, baba yake akamwona, moyo wake ukajawa na huruma. Akamkimbilia mwanawe, akamkumbatia na kumbusu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo akaondoka na kurudi kwa baba yake. Alipokuwa mbali na nyumbani kwao, baba yake alimwona, akamwonea huruma. Akamkimbilia, akamkumbatia na kumbusu sana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, akaanza safari ya kurudi kwa baba yake. Alipokuwa bado yu mbali, baba yake alimwona, na kwa moyo wa huruma alimkimbilia, akamkumbatia na kumbusu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, akaanza safari ya kurudi kwa baba yake. Alipokuwa bado yu mbali, baba yake alimwona, na kwa moyo wa huruma alimkimbilia, akamkumbatia na kumbusu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi akaondoka, akaenda kwa baba yake. “Lakini alipokuwa bado yuko mbali, baba yake akamwona, moyo wake ukajawa na huruma. Akamkimbilia mwanawe, akamkumbatia na kumbusu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi akaondoka, akaenda kwa baba yake. “Lakini alipokuwa bado yuko mbali, baba yake akamwona, moyo wake ukajawa na huruma. Akamkimbilia mwanawe, akamkumbatia na kumbusu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa bado mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, akaanza safari ya kurudi kwa baba yake. Alipokuwa bado yu mbali, baba yake alimwona, na kwa moyo wa huruma alimkimbilia, akamkumbatia na kumbusu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akaondoka, akaenda kwa baba yake. Akingali mbali bado, baba yake akamwona, akamwonea uchungu, akapiga mbio, akamkumbatia shingoni, akamnonea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akafunga safari yake na kurudia kwa baba yake. “Alipokuwa angali mbali kidogo, baba yake akamwona, akamusikilia huruma. Akamukimbilia, akamukumbatia mwana wake na kumubusu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akaondoka, akaenda kwa baba yake. Alipokuwa angali mbali, baba yake akamwona, akamhurumia, akapiga mbio, akamwangukia shingoni, akambusu sana.