Luke 15:29 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini yeye akamjibu: ‘Kumbuka! Miaka yote nimekutumikia, sijavunja amri yako hata mara moja. Umenipa nini? Hujanipa hata mwanambuzi mmoja nikafanye sherehe pamoja na rafiki zangu!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini yeye akamjibu baba yake, ‘Tazama! Miaka yote hii nimekutumikia na hata siku moja sijaacha kutii amri zako, lakini hujanipa hata mwana-mbuzi ili nifurahi na rafiki zangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini alimwambia baba yake, ‘Tazama, miaka yote hii nimekutumikia kama mtumishi, kamwe sijaacha kukutii! Lakini hujawahi kunipa hata mbuzi mdogo ili nisherehekee pamoja na rafiki zangu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini yeye akamjibu: Kumbuka! Miaka yote nimekutumikia, sijavunja amri yako hata mara moja. Umenipa nini? Hujanipa hata mwana mbuzi mmoja nikafanye sherehe pamoja na rafiki zangu!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini yeye akamjibu: ‘Kumbuka! Miaka yote nimekutumikia, sijavunja amri yako hata mara moja. Umenipa nini? Hujanipa hata mwanambuzi mmoja nikafanye sherehe pamoja na rafiki zangu!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini yeye akamjibu baba yake, ‘Tazama! Miaka yote hii nimekutumikia na hata siku moja sijaacha kutii amri zako, lakini hujanipa hata mwana mbuzi ili nifurahi na rafiki zangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini yeye akamjibu baba yake, ‘Tazama! Miaka yote hii nimekutumikia na hata siku moja sijaacha kutii amri zako, lakini hujanipa hata mwana-mbuzi ili nifurahi na rafiki zangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wowote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nisherehekee na rafiki zangu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini yeye akamjibu: ‘Kumbuka! Miaka yote nimekutumikia, sijavunja amri yako hata mara moja. Umenipa nini? Hujanipa hata mwanambuzi mmoja nikafanye sherehe pamoja na rafiki zangu!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akamjibu baba yake akimwambia: Tazama, miaka hii yote ninakutumikia; tena hakuna agizo lako, nisilolifanya. Nawe hujanipa hata kibuzi, nipate kushangilia na rafiki zangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini akamujibu baba yake: ‘Ninakutumikia kwa miaka mingi na sijakukosea hata mara moja. Ingawa vile haujanipatia hata kitoto cha mbuzi kusudi nifurahi pamoja na warafiki zangu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akamjibu baba yake akamwambia, Tazama, mimi nimekutumikia hii miaka mingapi: wala sikukhalifu amri yako wakati wo wote wala hukunipa mimi mwana mbuzi wakati wo wote illi nifurahi pamoja na rafiki zangu.