Luke 15:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Hivi, mmoja wenu akiwa na kondoo 100, akigundua kwamba mmoja wao amepotea, atafanya nini? Atawaacha wale tisini na tisa mbugani, na kwenda kumtafuta yule aliyepotea mpaka ampate.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ikiwa mmoja wenu ana kondoo mia moja, naye akapoteza mmoja wao, je, hawaachi wale tisini na tisa nyikani na kwenda kumtafuta huyo aliyepotea hadi ampate?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Chukulia mmoja wenu ana kondoo mia, lakini mmoja akapotea. Utafanya nini? Utawaacha wale tisini na tisa na kwenda kumtafuta yule mmoja aliyepotea mpaka umpate.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Hivi, mtu akiwa na kondoo mia, akigundua kwamba mmoja wao amepotea, atafanya nini? Atawaacha wale tisini na tisa mbugani, na kwenda kumtafuta yule aliyepotea mpaka ampate.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Hivi, mmoja wenu akiwa na kondoo 100, akigundua kwamba mmoja wao amepotea, atafanya nini? Atawaacha wale tisini na tisa mbugani, na kwenda kumtafuta yule aliyepotea mpaka ampate.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ikiwa mmoja wenu ana kondoo mia moja naye akapoteza mmoja wao, je, hawaachi wale tisini na tisa nyikani na kwenda kumtafuta huyo aliyepotea mpaka ampate?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ikiwa mmoja wenu ana kondoo mia moja, naye akapoteza mmoja wao, je, hawaachi wale tisini na tisa nyikani na kwenda kumtafuta huyo aliyepotea mpaka ampate?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na tisa nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hadi amwone?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Hivi, mmoja wenu akiwa na kondoo 100, akigundua kwamba mmoja wao amepotea, atafanya nini? Atawaacha wale tisini na tisa mbugani, na kwenda kumtafuta yule aliyepotea mpaka ampate.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwenu yuko mtu mwenye kondoo mia akipoteza mmoja wao, asiyewaacha wale tisini na tisa porini, aende kumtafuta yule aliyepotea, mpaka atakapomwona?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ni nani kati yenu akiwa na kondoo mia moja, na mumoja wao akipotea, atakayekosa kuwaacha wale wengine makumi tisa na tisa kwenye mashamba ya kulishia wanyama na kwenda kumutafuta yule aliyepotea mpaka atakapomupata?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mtu gani wenu aliye na kondoo mia, akipotewa na mmoja, asiyewaacha wale tissa na tissaini jangwani, na kumwendea yule aliyepotea, hatta atakapomwona?