Luke 15:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Au mwaonaje? Tuseme mwanamke fulani ana sarafu kumi za fedha, akipoteza moja, atafanya nini? Atawasha taa, ataifagia nyumba na kuitafuta kwa uangalifu mpaka aipate.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Au ikiwa mwanamke ana sarafu za fedha kumi, naye akapoteza moja, je, hawashi taa na kufagia nyumba na kuitafuta kwa bidii hadi aipate?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Fikiria kuhusu mwanamke mwenye sarafu kumi za fedha, lakini akapoteza sarafu moja kati ya hizo. Atawasha taa na kuifagia nyumba. Ataitafuta sarafu kwa bidii mpaka aione.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Au mwaonaje? Tuseme mwanamke fulani ana sarafu kumi za fedha, akipoteza moja, atafanya nini? Atawasha taa, aifagie nyumba na kuitafuta kwa uangalifu mpaka aipate.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Au mwaonaje? Tuseme mwanamke fulani ana sarafu kumi za fedha, akipoteza moja, atafanya nini? Atawasha taa, ataifagia nyumba na kuitafuta kwa uangalifu mpaka aipate.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Au ikiwa mwanamke ana sarafu za fedha kumi, naye akapoteza moja, je, hawashi taa na kufagia nyumba na kuitafuta kwa bidii mpaka aipate?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Au ikiwa mwanamke ana sarafu za fedha kumi, naye akapoteza moja, je, hawashi taa na kufagia nyumba na kuitafuta kwa bidii mpaka aipate?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Au ni mwanamke gani aliye na shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hadi aione?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Au mwaonaje? Tuseme mwanamke fulani ana sarafu kumi za fedha, akipoteza moja, atafanya nini? Atawasha taa, ataifagia nyumba na kuitafuta kwa uangalifu mpaka aipate.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Au yuko mwanamke mwenye shilingi kumi akipoteza moja, asiyewasha taa na kufagia nyumbani na kuitafuta kwa uangalifu, mpaka atakapoiona?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Vilevile ni mwanamuke gani anayekuwa na vikoroti kumi vya feza, naye akipoteza kimoja, atakayekosa kuwakisha taa na kufagia nyumba kutafuta vizuri mpaka akipate?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ama mwanamke gani aliye na rupia kumi, akipotewa na rupia mmoja, asiyewasha taa, na kuifagia nyumba, akitatuta kwa bidii, hatta atakapoiona?