Luke 16:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeyote aliye mwaminifu katika mambo madogo, atakuwa mwaminifu katika mambo makubwa; na yeyote asiye mwaminifu katika mambo madogo, hatakuwa mwaminifu katika mambo makubwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Yeyote aliye mwaminifu katika mambo madogo, pia ni mwaminifu katika mambo makubwa. Na yeyote asiye mwaminifu katika mambo madogo pia si mwaminifu katika mambo makubwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtu yeyote anayeweza kuaminiwa kwa mambo madogo anaweza kuaminiwa kwa mambo makubwa pia. Mtu asiye mwaminifu katika jambo dogo hawezi kuwa mwaminifu katika jambo kubwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yeyote aliye mwaminifu katika mambo madogo, atakuwa mwaminifu katika mambo makubwa; na yeyote asiye mwaminifu katika mambo madogo, hatakuwa mwaminifu katika mambo makubwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeyote aliye mwaminifu katika mambo madogo, atakuwa mwaminifu katika mambo makubwa; na yeyote asiye mwaminifu katika mambo madogo, hatakuwa mwaminifu katika mambo makubwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ye yote aliye mwaminifu katika mambo madogo, pia ni mwaminifu hata katika mambo makubwa, naye mtu ambaye si mwaminifu katika mambo madogo pia si mwaminifu katika mambo makubwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Yeyote aliye mwaminifu katika mambo madogo, pia ni mwaminifu hata katika mambo makubwa, naye mtu ambaye si mwaminifu katika mambo madogo pia si mwaminifu katika mambo makubwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na asiyeaminika katika lililo dogo, huwa haaminiki pia katika lililo kubwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeyote aliye mwaminifu katika mambo madogo, atakuwa mwaminifu katika mambo makubwa; na yeyote asiye mwaminifu katika mambo madogo, hatakuwa mwaminifu katika mambo makubwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Aliye mwelekevu wa vitu vilivyo vichache huwa mwelekevu hata wa vile vilivyo vingi. Naye aliye mpotovu wa vitu vilivyo vichache huwa mpotovu hata wa vile vilivyo vingi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule anayekuwa mwaminifu katika vitu vichache, yuko mwaminifu vilevile katika vitu vingi. Na yule asiyekuwa mwaminifu katika vitu vichache, hayuko mwaminifu vilevile katika vitu vingi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Aliye mwaminifu katika kile kilicho kidogo huwa mwaminifu na katika kile kilicho kikubwa: nae aliye mdhalimu katika kile kilicho kidogo, huwa mdhalimu na katika kile kilicho kikubwa.