Luke 16:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Sheria na maandishi ya manabii vilikuwako mpaka wakati wa Yohane Mbatizaji. Tangu hapo, ufalme wa Mungu unahubiriwa, na kila mmoja anauingia kwa nguvu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Torati na Manabii vilihubiriwa hadi kuja kwa Yahya. Tangu wakati huo Injili ya ufalme wa Mungu inahubiriwa, na kila mmoja hujiingiza kwa nguvu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kabla ya Yohana Mbatizaji kuja, watu walifundishwa Sheria ya Musa na maandishi ya Manabii. Lakini tangu wakati wa Yohana, Habari Njema kuhusu ufalme wa Mungu inahubiriwa. Na kila mtu anajitahidi sana ili kuingia katika ufalme wa Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Sheria na maandishi ya manabii vilikuweko mpaka wakati wa Yohane mbatizaji. Tangu hapo, Ufalme wa Mungu unahubiriwa, na kila mmoja anauingia kwa nguvu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Sheria na maandishi ya manabii vilikuwako mpaka wakati wa Yohane Mbatizaji. Tangu hapo, ufalme wa Mungu unahubiriwa, na kila mmoja anauingia kwa nguvu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Torati na manabii vilitumiwa mpaka kuja kwa Yohana Mbatizaji. Tangu wakati huo habari njema za Ufalme wa Mungu zinahubiriwa na kila mmoja hujiingiza kwa nguvu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Torati na Manabii vilihubiriwa mpaka kuja kwa Yahya. Tangu wakati huo habari njema za Ufalme wa Mwenyezi Mungu zinahubiriwa, na kila mmoja hujiingiza kwa nguvu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Torati na Manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo Habari Njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Sheria na maandishi ya manabii vilikuwako mpaka wakati wa Yohane Mbatizaji. Tangu hapo, ufalme wa Mungu unahubiriwa, na kila mmoja anauingia kwa nguvu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mambo ya Maonyo na ya Wafumbuaji yametangazwa mpaka kuja kwake Yohana; toka hapo hutangazwa Utume mwema wa ufalme wa Mungu, tena kila mtu huingizwa kwa nguvu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Sheria ya Musa na maandiko ya manabii yalitangazwa mpaka kuja kwa Yoane. Tangu wakati ule, Habari Njema ya Ufalme wa Mungu inahubiriwa, na kila mutu anajiingiza kwa kinguvu ndani ya ufalme ule.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Torati na manabii zilikuwako mpaka Yohana. Tangu wakati ule, khabari njema ya ufalme wa Mungu inakhubiriwa, na killa mtu anauingia kwa nguvu.