Luke 16:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule tajiri akamwita, akamwambia: ‘Ni mambo gani haya ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya mapato na matumizi ya mali yangu, kwa maana huwezi kuwa karani tena.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo huyo tajiri akamwita na kumuuliza, ‘Ni mambo gani haya ninayoyasikia kukuhusu? Toa taarifa ya usimamizi wako, kwa sababu huwezi kuendelea kuwa msimamizi.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamwita, akamwambia, Ni habari gani hii ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya uwakili wako, kwa kuwa huwezi kuwa wakili tena.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo, akamwita, akamwambia, ‘Nimesikia mambo mabaya juu yako. Nipe taarifa namna ulivyosimamia pesa zangu. Huwezi kuendelea kuwa msimamizi wangu.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yule tajiri akamwita akamwambia: Ni mambo gani haya ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya mapato na matumizi ya mali yangu, kwa maana huwezi kuwa karani tena.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule tajiri akamwita, akamwambia: ‘Ni mambo gani haya ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya mapato na matumizi ya mali yangu, kwa maana huwezi kuwa karani tena.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo huyo tajiri akamwita na kumwuliza, ‘Ni mambo gani haya ninayoyasikia kukuhusu? Toa taarifa ya usimamizi wako, kwa sababu huwezi kuendelea kuwa msimamizi.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo huyo tajiri akamwita na kumuuliza, ‘Ni mambo gani haya ninayoyasikia kukuhusu? Toa taarifa ya usimamizi wako, kwa sababu huwezi kuendelea kuwa msimamizi.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamwita, akamwambia, Ni habari gani hii ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya uwakili wako, kwa kuwa huwezi kuwa wakili tena.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule tajiri akamwita, akamwambia: ‘Ni mambo gani haya ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya mapato na matumizi ya mali yangu, kwa maana huwezi kuwa karani tena.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akamwita, akamwambia: Hayo nayasikiaje kwako? Toa hesabu ya utunzaji wako wa mali zangu! Kwani huwezi tena kuzitunza mali zangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamwita, akamwambia, Ni habari gani hii ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya uwakili wako, kwa kuwa huwezi kuwa wakili tena.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu bwana wake akamwita na kumwambia: ‘Ni habari gani ile waliyonielezea juu yako? Ninakuomba unifanyie hesabu yote ya mali yangu, kwa sababu hauwezi tena kuwa mulinzi wa mali yangu.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akamwita, akamwambia, Nini hii nisikiayo juu yako? Toa khabari ya uwakili wako, maana huwezi tena kuwa wakili.