Luke 16:21 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lazaro alitamani kupewa makombo yaliyoanguka kutoka mezani pa huyo tajiri; na zaidi ya hayo, mbwa walikuwa wanakuja na kuramba vidonda vyake!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huyo Lazaro alitamani kujishibisha kwa makombo yaliyoanguka kutoka mezani kwa yule tajiri. Hata mbwa walikuwa wakija na kuramba vidonda vyake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lazaro alitaka tu kula masalia ya vyakula vilivyokuwa sakafuni vilivyodondoka kutoka mezani kwa tajiri. Na mbwa walikuja na kulamba vidonda vyake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lazaro alitamani kula makombo yaliyoanguka kutoka meza ya tajiri; na zaidi ya hayo, mbwa walikuwa wanakuja na kulamba vidonda vyake!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lazaro alitamani kupewa makombo yaliyoanguka kutoka mezani pa huyo tajiri; na zaidi ya hayo, mbwa walikuwa wanakuja na kuramba vidonda vyake!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huyo Lazaro alitamani kujishibisha kwa makombo yaliyoanguka kutoka mezani kwa yule tajiri. Hata mbwa walikuwa wakija na kulamba vidonda vyake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huyo Lazaro alitamani kujishibisha kwa makombo yaliyoanguka kutoka mezani kwa yule tajiri. Hata mbwa walikuwa wakija na kuramba vidonda vyake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa walikuwa wakija na kumramba vidonda vyake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lazaro alitamani kupewa makombo yaliyoanguka kutoka mezani pa huyo tajiri; na zaidi ya hayo, mbwa walikuwa wanakuja na kuramba vidonda vyake!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akataka sana kushibishwa na makombo yaliyoanguka mezani pake mwenye mali; mbwa nao huja kumlamba vidonda vyake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeye alikuwa akitamani kula makombo yaliyoanguka toka juu ya meza ya yule tajiri. Hata imbwa walikuja kulambulalambula vile vidonda vyake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akitamani kushibishwa na makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri: hatta mbwa nao huja, humramba vidonda vyake.