Luke 16:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo tajiri, akiwa na mateso makali huko kuzimu, akainua macho yake, akamwona Abrahamu kwa mbali na Lazaro karibu naye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kule Kuzimu alipokuwa akiteseka, alitazama juu, akamwona Ibrahimu kwa mbali, naye Lazaro alikuwa kifuani mwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alichukuliwa mpaka mahali pa mauti na akawa katika maumivu makuu. Alimwona Ibrahimu kwa mbali na Lazaro akiwa kifuani pake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Huyo tajiri, alikuwa na mateso makali huko kuzimu, akainua macho yake, akamwona Abrahamu kwa mbali na Lazaro karibu naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo tajiri, akiwa na mateso makali huko kuzimu, akainua macho yake, akamwona Abrahamu kwa mbali na Lazaro karibu naye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kule kuzimu alipokuwa akiteseka, alitazama juu, akamwona Abrahamu kwa mbali, naye Lazaro alikuwa karibu yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kule kuzimu alipokuwa akiteseka, alitazama juu, akamwona Ibrahimu kwa mbali, naye Lazaro alikuwa karibu yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Abrahamu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo tajiri, akiwa na mateso makali huko kuzimu, akainua macho yake, akamwona Abrahamu kwa mbali na Lazaro karibu naye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipokuwa kuzimuni katika maumivu akayainua macho yake, akamwona Aburahamu, yuko mbali, naye Lazaro alikuwa amekaa kifuani pake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alipokuwa katika jehenamu akiteswa sana, akainua macho, akamwona Abrahamu kwa mbali na Lazaro akiwa pembeni yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi katika akhera akainua macho yake, akiwa katika adhabu, akamwona Ibrahimu yuko mbali, na Lazaro kifuani pake.