Luke 16:24 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, akaita kwa sauti: ‘Babu Abrahamu, nionee huruma; umtume Lazaro angalau achovye ncha ya kidole chake katika maji, auburudishe ulimi wangu, maana ninateseka mno katika moto huu.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo yule tajiri akamwita, ‘Baba Ibrahimu, nihurumie na umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake ndani ya maji aupoze ulimi wangu, kwa sababu nina maumivu makuu kwenye moto huu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Akaita, ‘Baba Ibrahimu, nihurumie! Mtume Lazaro kwangu ili achovye ncha ya kidole chake kwenye maji na kuupoza ulimi wangu, kwa sababu ninateseka katika moto huu!’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, akaita kwa sauti: Baba Abrahamu, nionee huruma; umtume Lazaro angalau achovye ncha ya kidole chake katika maji, auburudishe ulimi wangu, maana ninateseka mno katika moto huu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, akaita kwa sauti: ‘Babu Abrahamu, nionee huruma; umtume Lazaro angalau achovye ncha ya kidole chake katika maji, auburudishe ulimi wangu, maana ninateseka mno katika moto huu.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo yule tajiri akamwita, ‘Baba Abrahamu, nihurumie na umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake ndani ya maji aupoze ulimi wangu, kwa sababu nina maumivu makuu kwenye moto huu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo yule tajiri akamwita, ‘Baba Ibrahimu, nihurumie na umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake ndani ya maji aupoze ulimi wangu, kwa sababu nina maumivu makuu kwenye moto huu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akalia, akasema, Ee baba Abrahamu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, aupoze ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, akaita kwa sauti: ‘Babu Abrahamu, nionee huruma; umtume Lazaro angalau achovye ncha ya kidole chake katika maji, auburudishe ulimi wangu, maana ninateseka mno katika moto huu.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaita akisema: Baba Aburahamu, nihurumie! Umtume Lazaro, achovye ncha ya kidole chake majini, aje, aupoze ulimi wangu! kwani naumia humu motoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi akalalamika, akisema: ‘Baba Abrahamu, unisikilie huruma; umutume Lazaro achovye incha ya kidole chake katika maji, anipoleshe ulimi wangu, kwa sababu ninateswa sana katika moto huu.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akalia, akasema, Baba Ibrahimu, unirehemu, umtume Lazaro, achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa maana naumia katika moto huu.