Luke 16:31 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Abrahamu akasema: ‘Kama hawawasikilizi Mose na manabii, hawatajali hata kama mtu angefufuka kutoka kwa wafu.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ibrahimu akamwambia, ‘Kama wasipowasikiliza Musa na Manabii, hawataweza kushawishika hata kama mtu akifufuka kutoka kwa wafu.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Ibrahimu akamwambia, ‘Ikiwa ndugu zako hawatawasikiliza Musa na manabii, hawataweza kumsikiliza mtu yeyote kutoka kwa wafu.’”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye Abrahamu akasema: Kama hawawasikilizi Mose na manabii, hawatajali hata kama mtu angefufuka kutoka wafu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Abrahamu akasema: ‘Kama hawawasikilizi Mose na manabii, hawatajali hata kama mtu angefufuka kutoka kwa wafu.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Abrahamu akamwambia, ‘Kama wasipowasikiliza Mose na manabii, hawataweza kushawishiwa hata kama atafufuka mtu kutoka kwa wafu.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ibrahimu akamwambia, ‘Kama wasipowasikiliza Musa na Manabii, hawataweza kushawishika hata kama mtu akifufuka kutoka kwa wafu.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishika hata mtu akifufuka katika wafu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Abrahamu akasema: ‘Kama hawawasikilizi Mose na manabii, hawatajali hata kama mtu angefufuka kutoka kwa wafu.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini akamwambia: Wasipomsikia Mose na Wafumbuaji hawataonyeka, hata mtu akifufuka katika wafu.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Abrahamu akamwambia: ‘Kama wandugu zako hawasikilizi maonyo ya Musa na ya manabii, hawatasadiki hata mutu aliyefufuka.’ ”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akamwambia, Wasiposikia Musa na manabii, ajapoondoka mtu katika wafu, hawatashawishwa.