Luke 16:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naam, najua la kufanya, ili nitakapofukuzwa kazi, watu waweze kunikaribisha nyumbani kwao.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Najua nitakalofanya ili nikiachishwa kazi yangu hapa, watu wanikaribishe nyumbani mwao.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Najua nitakalotenda, ili nitakapotolewa katika uwakili, wanikaribishe nyumbani mwao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Najua nitakalofanya! Nitafanya kitu nipate marafiki. Ili nitakapopoteza kazi yangu, watanikaribisha katika nyumba zao.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naam, najua la kufanya, ili nitakapofukuzwa kazi, watu waweze kunikaribisha nyumbani kwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naam, najua la kufanya, ili nitakapofukuzwa kazi, watu waweze kunikaribisha nyumbani kwao.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Najua nitakalofanya ili nikiachishwa kazi yangu hapa, watu wanikaribishe nyumbani kwao.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Najua nitakalofanya ili nikiachishwa kazi yangu hapa, watu wanikaribishe nyumbani kwao.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Najua nitakalotenda, ili nitakapotolewa katika uwakili, wanikaribishe nyumbani mwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naam, najua la kufanya, ili nitakapofukuzwa kazi, watu waweze kunikaribisha nyumbani kwao.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nimetambua, nitakavyofanya, kusudi wanipokee nyumbani mwao, nitakapoondolewa katika utunzaji wa mali.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Najua nitakalotenda, ili nitakapotolewa katika uwakili, wanikaribishe nyumbani mwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa ninajua jinsi nitakavyofanya kusudi wakati nitafukuzwa kwa kazi yangu ya ulinzi, watu wapate kunikaribisha katika nyumba zao.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nimekwisha kujua nitakalotenda, illi, nitolewapo katika nwakili, wanikaribishe nyumbani mwao.