Luke 16:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akamwuliza mdeni mwingine: ‘Wewe unadaiwa kiasi gani?’ Yeye akamjibu: ‘Magunia 100 ya ngano.’ Yule karani akamwambia: ‘Chukua hati yako ya deni, andika themanini.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kisha akamuuliza wa pili, ‘Wewe deni lako ni kiasi gani?’ “Akajibu, ‘Vipimo elfu moja vya ngano.’ “Yule msimamizi akamwambia, ‘Chukua hati yako, uandike vipimo mia nane!’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akamwambia mwingine, Na wewe wawiwani? Akasema, Makanda mia ya ngano. Akamwambia, Twaa hati yako, andika themanini.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha akamwambia mwingine, ‘Na wewe kiasi gani unadaiwa?’ Akajibu, ‘Vipimo mia moja vya ngano.’ Akamwambia, ‘Chukua hati yako ya deni, ibadilishe iwe vipimo themanini.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha akamwuliza mdeni mwingine: Wewe unadaiwa kiasi gani? Yeye akamjibu: Magunia mia ya ngano. Yule karani akamwambia: Chukua hati yako ya deni, andika themanini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akamwuliza mdeni mwingine: ‘Wewe unadaiwa kiasi gani?’ Yeye akamjibu: ‘Magunia 100 ya ngano.’ Yule karani akamwambia: ‘Chukua hati yako ya deni, andika themanini.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kisha akamwuliza wa pili, ‘Wewe deni lako ni kiasi gani?’ “Akajibu, ‘Vipimo 1,000 vya ngano.’ “Yule msimamizi akamwambia, ‘Chukua hati yako, andika vipimo 800!’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kisha akamuuliza wa pili, ‘Wewe deni lako ni kiasi gani?’ “Akajibu, ‘Vipimo 1,000 vya ngano.’ “Yule msimamizi akamwambia, ‘Chukua hati yako, andika vipimo 800!’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akamwambia mwingine, Na wewe unadaiwa nini? Akasema, Makanda mia ya ngano. Akamwambia, Twaa hati yako, andika themanini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha akamwuliza mdeni mwingine: ‘Wewe unadaiwa kiasi gani?’ Yeye akamjibu: ‘Magunia 100 ya ngano.’ Yule karani akamwambia: ‘Chukua hati yako ya deni, andika themanini.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akamwambia mwingine: Na wewe una deni gani? Naye aliposema: Makanda 100 ya mchele, akamwambia: Kichukue cheti chako, uandike 80!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akamwambia mwingine, Na wewe wawiwani? Akasema, Makanda mia ya ngano. Akamwambia, Twaa hati yako, andika themanini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akamwuliza mwingine: ‘Na wewe uko na deni yapata gani?’ Naye akajibu: ‘Saki mia moja za ngano.’ Yule mulinzi akamwambia: ‘Kamata barua yako ya mapatano na uandike saki makumi nane.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akiisha, akamwambia mwingine, Na wewe wawiwani? Akasema, Mikanda mia ya nganu. Akamwambia, Twaa khati yako, andika themanini.