Luke 16:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Yesu akaendelea kusema, “Nami nawaambieni, jifanyieni marafiki kutokana na mali ya dunia, ili zitakapowaishieni, wawapokeeni katika makao ya milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nawaambia, tumieni mali ya dunia kujipatia rafiki, ili itakapokwisha, mkaribishwe katika makao ya milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nawaambia, Jifanyieni rafiki kwa mali ya udhalimu, ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninamaanisha hivi: Vitumieni vitu vya kidunia mlivyonavyo sasa ili muwe na ‘marafiki’ kwa ajili ya siku za baadaye. Ili wakati vitu hivyo vitakapotoweka, mtakaribishwa katika nyumba ya milele.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye Yesu akaendelea kusema, “Nami nawaambieni, jifanyieni marafiki kutokana na mali ya dunia, ili zitakapowaishieni, mweze kupokewa nao katika makao ya milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Yesu akaendelea kusema, “Nami nawaambieni, jifanyieni marafiki kutokana na mali ya dunia, ili zitakapowaishieni, wawapokeeni katika makao ya milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nawaambia, tumieni mali ya kidunia kujipatia marafiki, ili itakapokwisha, mkaribishwe katika makao ya milele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nawaambia, tumieni mali ya kidunia kujipatia marafiki, ili itakapokwisha, mkaribishwe katika makao ya milele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nawaambia, Jifanyieni rafiki kwa mali ya duniani, ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Yesu akaendelea kusema, “Nami nawaambieni, jifanyieni marafiki kutokana na mali ya dunia, ili zitakapowaishieni, wawapokeeni katika makao ya milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nami nawaambiani: Jipatieni rafiki na kutoa mali za nchini zilizo za upotovu, kusudi wawapokee kwenye makao ya kale na kale, mali zitakapokoseka!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nawaambia, Jifanyieni rafiki kwa mali ya udhalimu, ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akaongeza kusema: “Nami ninawaambia: mutumie mali ya dunia hii kwa kuunga urafiki, kusudi wakati mali ile itakapokosekana, mupate kupokelewa kwenye makao ya milele.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na mimi nawaambia ninyi, Jifanyieni rafiki kwa mamona ya udhalimu, illi itakapopunguka wawakaribishe ninyi katika makao ya milele.