Luke 17:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Haiwezekani kabisa kusitokee vikwazo vinavyosababisha dhambi; lakini ole wake mtu yule atakayevisababisha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akawaambia wanafunzi wake, “Mambo yanayosababisha watu watende dhambi hayana budi kutukia. Lakini ole wake mtu yule anayeyasababisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake!
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akawaambia wafuasi wake, “Mambo yanayosababisha watu kutenda dhambi yatatokea hakika. Lakini ole wake mtu anayesababisha hili litokee.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha, Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Haiwezekani kabisa kusitokee vikwazo vinavyosababisha dhambi; lakini ole wake mtu yule atakayevisababisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Haiwezekani kabisa kusitokee vikwazo vinavyosababisha dhambi; lakini ole wake mtu yule atakayevisababisha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mambo yasababishayo watu watende dhambi hayana budi kutukia. Lakini ole wake mtu yule anayeyasababisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akawaambia wanafunzi wake, “Mambo yanayosababisha watu watende dhambi hayana budi kutukia. Lakini ole wake mtu yule anayeyasababisha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia wanafunzi wake, Vikwazo havina budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye vinakuja kwa sababu yake!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Haiwezekani kabisa kusitokee vikwazo vinavyosababisha dhambi; lakini ole wake mtu yule atakayevisababisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akawaambia wanafunzi wake: Makwazo hayana budi kuja, lakini anayeyaleta atapatwa na mambo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akawaambia wanafunzi wake: “Sherti mambo ya kuwaangusha watu yatokee, lakini ole kwa mutu yule anayeyaleta!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
AKAWAAMBIA wanafunzi wake, Mambo ya kukosesha hayana buddi kutokea, lakini ole wake mtu yule ayaletae!