Luke 17:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hali kadhalika na nyinyi mkisha fanya yote mliyoamriwa, semeni: ‘Sisi ni watumishi tusio na faida, tumetimiza tu yale tuliyotakiwa kufanya.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vivyo hivyo nanyi mkishafanya mliyoagizwa, semeni, ‘Sisi tu watumishi tusiostahili; tumefanya tu yale tuliyopaswa kufanya.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Vivyo hivyo nanyi. Mkimaliza kufanya yote mliyoamriwa kufanya, mseme, ‘Sisi ni watumwa, hatustahili shukrani yoyote maalumu. Tumefanya kazi tunayotakiwa kufanya.’”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hali kadhalika na ninyi mkisha fanya yote mliyoamriwa, semeni: Sisi ni watumishi tusio na faida, tumetimiza tu yale tuliyotakiwa kufanya.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hali kadhalika na nyinyi mkisha fanya yote mliyoamriwa, semeni: ‘Sisi ni watumishi tusio na faida, tumetimiza tu yale tuliyotakiwa kufanya.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vivyo hivyo nanyi mkiisha kufanya mliyoagizwa, semeni, ‘Sisi tu watumishi tusiostahili; tumefanya tu yale tuliyopaswa kufanya.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vivyo hivyo nanyi mkiisha kufanya mliyoagizwa, semeni, ‘Sisi tu watumishi tusiostahili; tumefanya tu yale tuliyopaswa kufanya.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hali kadhalika na nyinyi mkisha fanya yote mliyoamriwa, semeni: ‘Sisi ni watumishi tusio na faida, tumetimiza tu yale tuliyotakiwa kufanya.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vivyo nanyi matakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa semeni: Sisi tu watumwa wasiofaa, tumefanya tu yaliyotupasa kuyafanya!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na ni hivi inavyokuwa kwenu vilevile. Wakati mutakapokwisha kufanya yote muliyoamuriwa, museme: ‘Sisi ni watumishi tu, tumetimiza tu mapaswa yetu.’ ”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kadhalika na ninyi, mkiisha kufanya vyote mlivyoamriwa, semeni, Sisi watumishi wasiofaa; tumetenda yaliyotupasa kutenda.