Luke 17:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ingekuwa afadhali kwake kufungiwa shingoni jiwe kubwa la kusagia na kutoswa baharini, kuliko kumkwaza mmoja wa wadogo hawa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ingekuwa heri kama mtu huyo angefungiwa jiwe la kusagia shingoni na kutoswa baharini, kuliko kumsababisha mmoja wa hawa wadogo kutenda dhambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ingekuwa vizuri kwa mtu huyo kama jiwe la kusagia lingefungwa shingoni mwake, na akatupwa baharini, kuliko kusababisha mmojawapo wa wanyenyekevu hawa kutenda dhambi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ingekuwa afadhali kwake kufungiwa shingoni jiwe kubwa la kusagia na kutoswa baharini, kuliko kumkwaza mmoja wa wadogo hawa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ingekuwa afadhali kwake kufungiwa shingoni jiwe kubwa la kusagia na kutoswa baharini, kuliko kumkwaza mmoja wa wadogo hawa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ingekuwa heri kama mtu huyo angefungiwa jiwe zito la kusagia shingoni na kutoswa baharini kuliko kumfanya mmoja wa hawa wadogo atende dhambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ingekuwa heri kama mtu huyo angefungiwa jiwe la kusagia shingoni na kutoswa baharini, kuliko kumsababisha mmojawapo wa hawa wadogo kutenda dhambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ingekuwa afadhali kwake kufungiwa shingoni jiwe kubwa la kusagia na kutoswa baharini, kuliko kumkwaza mmoja wa wadogo hawa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akitundikwa shingoni pake jiwe kubwa la kusagia, kisha atumbukizwe baharini, inamfaa kuliko kukwaza mmoja tu aliye mwenzao hawa wadogo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ingekuwa heri afungiwe jiwe kubwa la kusagia katika shingo na kutumbukizwa ndani ya bahari, kuliko kumwangusha mumoja wa wadogo hawa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ingemfaa huyu zaidi jiwe la kusagia litiwe shingoni pake akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa hawa wadogo.