Luke 17:31 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Siku hiyo, yeyote atakayekuwa juu ya paa asishuke kwenda nyumbani kuchukua mali yake. Kadhalika, naye atakayekuwa shambani asirudi nyuma.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku hiyo, mtu yeyote aliye juu ya dari ya nyumba yake, hata vitu vyake vikiwa ndani ya hiyo nyumba, asishuke kuvichukua. Vivyo hivyo mtu aliye shambani asirudi nyumbani kuchukua chochote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika siku ile, aliye juu ya dari, na vyombo vyake vimo ndani ya nyumba, asishuke ili kuvitwaa; na kadhalika, aliye shambani asirejee nyuma.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Siku hiyo, ikiwa mtu atakuwa juu ya paa ya nyumba yake, hatakuwa na muda wa kushuka kwenda ndani ya nyumba kuchukua vitu vyake. Ikiwa atakuwa shambani, hataweza kurudi nyumbani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Siku hiyo, yeyote atakayekuwa juu ya paa asishuke nyumbani kuchukua mali yake. Kadhalika, naye atakayekuwa shambani asirudi nyuma.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Siku hiyo, yeyote atakayekuwa juu ya paa asishuke kwenda nyumbani kuchukua mali yake. Kadhalika, naye atakayekuwa shambani asirudi nyuma.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku hiyo, mtu ye yote aliyeko kwenye dari ya nyumba yake, vitu vyake vikiwa ndani ya hiyo nyumba asishuke kuvichukua. Vivyo hivyo mtu aliyeko shambani asirudi nyumbani kuchukua cho chote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku hiyo, mtu yeyote aliye juu ya dari ya nyumba yake, hata vitu vyake vikiwa ndani ya hiyo nyumba, asishuke kuvichukua. Vivyo hivyo mtu aliye shambani asirudi nyumbani kuchukua chochote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika siku ile, aliye juu ya dari, na mali yake imo ndani ya nyumba, asishuke ili kuitwaa; kadhalika, aliye shambani asirejee nyuma.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Siku hiyo, yeyote atakayekuwa juu ya paa asishuke kwenda nyumbani kuchukua mali yake. Kadhalika, naye atakayekuwa shambani asirudi nyuma.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ile mtu atakayekuwapo nyumbani juu, vitu vyake vikiwa nyumbani, asiingie kuvichukua! Vivyo hivyo naye atakayekuwako shambani asivirudie vilivyoko nyuma!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika siku ile, aliye juu ya dari, na vyombo vyake vimo ndani ya nyumba, asishuke ili kuvitwaa; na kadhalika, aliye shambani asirejee nyuma.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Siku ile, yule atakayekutiwa juu ya paa la nyumba, asishuke ndani yake kwa kukamata vitu vyake. Vilevile yule atakayekutiwa katika shamba, asirudie kwake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Katika siku ile, aliye juu darini, na vyombo vyake ndani ya nyumba, asishuke illi kuvitwaa: nae aliomo shambani vivyo hivyo asirejee nyuma.