Luke 17:37 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo wakamwuliza, “Ni wapi Bwana?” Naye akawaambia, “Palipo mzoga, ndipo tai watakapokusanyikia.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha wakamuuliza, “Haya yatatukia wapi Bwana Isa?” Akawaambia, “Pale ulipo mzoga, huko ndiko tai watakapokusanyika.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakajibu, wakamwuliza, Wapi, Bwana? Akawaambia, Ulipo mzoga, ndipo watakapokutanika tai.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wafuasi wake wakamuuliza, “Hii itakuwa wapi Bwana?” Yesu akajibu, “Ni kama kuutafuta mzoga, utaupata pale ambapo tai wamekusanyika.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo wakamwuliza, “Ni wapi Bwana?” Naye akawaambia, “Ulipo mzoga, ndipo tai watakapokusanyikia.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo wakamwuliza, “Ni wapi Bwana?” Naye akawaambia, “Palipo mzoga, ndipo tai watakapokusanyikia.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha wakamwuliza, “Haya yatatukia wapi Bwana?” Akawaambia, “Pale ulipo mzoga, ndipo tai watakapokusanyika.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha wakamuuliza, “Haya yatatukia wapi, Bwana Isa?” Akawaambia, “Pale ulipo mzoga, huko ndiko tai watakapokusanyika.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakajibu, wakamwuliza, Wapi, Bwana? Akawaambia, Ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo wakamwuliza, “Ni wapi Bwana?” Naye akawaambia, “Palipo mzoga, ndipo tai watakapokusanyikia.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipojibu na kumwuliza: Wapi, Bwana? akawaambia: Penye nyamafu ndipo, nao tai watakapokusanyikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakajibu, wakamwuliza, Wapi, Bwana? Akawaambia, Ulipo mzoga, ndipo watakapokutanika tai.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanafunzi wakamwuliza: “Bwana, mambo haya yatafanyika wapi?” Naye akawajibu: “Nafasi patakapokuwa muzoga ni pale tai watakapokusanyika.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakajibu wakamwambia, Wapi, Bwana? Akawaambia, Mzoga uliko ndiko watakakokutana tai.