Luke 17:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Bwana akajibu, “Kama imani yenu ingekuwa ndogo hata kama chembe ndogo ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu: ‘Ngoka ukajipandikize baharini,’ nao ungewatii.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Bwana akawajibu, “Kama mngekuwa na imani ndogo kama punje ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu, ‘Ng’oka ukaote baharini,’ nao ungewatii.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Bwana akasema, “Imani yenu ingekuwa kubwa kama mbegu ya haradali, mngeuambia mforosadi huu, ‘Ng'oka, ukajipandikize baharini,’ nao ungewatii.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye Bwana akajibu, “Kama imani yenu ingekuwa ndogo hata kama chembe ndogo ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu: Ng'oka ukajipandikize baharini, nao ungewatii.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Bwana akajibu, “Kama imani yenu ingekuwa ndogo hata kama chembe ndogo ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu: ‘Ng'oka ukajipandikize baharini,’ nao ungewatii.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akawajibu, “Kama mngekuwa na imani ndogo kama punje ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu, ‘Ng'oka ukaote baharini,’ Nao ungewatii.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Bwana Isa akawajibu, “Kama mkiwa na imani ndogo kama punje ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu, ‘Ng’oka ukaote baharini,’ nao ungewatii.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Bwana akajibu, “Kama imani yenu ingekuwa ndogo hata kama chembe ndogo ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu: ‘Ngoka ukajipandikize baharini,’ nao ungewatii.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana akasema: Cheo chenu cha kumtegemea Mungu kikiwa kidogo kama kipunje cha mbegu, mtauambia mkuyu huu: Ng'oka hapo, ulipo, ujipande baharini! nao utawatii.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng’oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bwana akajibu: “Kama mukiwa na imani, hata ikiwa tu kama punje ndogo sana ya haradali, mutaweza kuuambia muti huu wa mukuyu: ‘Ujiongoe hapa na uende kujipanda katika bahari,’ nao ungewatii.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bwana akasema, Mkiwa na imani kama punje ya kharadali, mngeuambia mzambarau huu, Ngʼoka ukapandwe baharini, nao ungewatiini.