Luke 17:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Tuseme mmoja wenu ana mtumishi ambaye analima shambani au anachunga kondoo. Je, anaporudi kutoka shambani, atamwambia huyo mtumishi: ‘Haraka, njoo ule chakula?’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ikiwa mmoja wenu ana mtumishi anayelima shambani au anayechunga kondoo, je, mtumishi huyo arudipo atamwambia, ‘Karibu hapa keti ule chakula’?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini, ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au achungaye ng'ombe, atakayemwambia mara arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule chakula?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Chukulia mmoja wenu ana mtumishi ambaye amekuwa shambani akilima au akichunga kondoo shambani. Akirudi kutoka shambani au machungani, utamwambia nini? Je, utamwambia, ‘Njoo ndani, keti, ule chakula’?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Tuseme mmoja wenu ana mtumishi ambaye analima shambani au anachunga kondoo. Je, anaporudi kutoka shambani, atamwambia: Haraka, njoo ule chakula?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Tuseme mmoja wenu ana mtumishi ambaye analima shambani au anachunga kondoo. Je, anaporudi kutoka shambani, atamwambia huyo mtumishi: ‘Haraka, njoo ule chakula?’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ikiwa mmoja wenu ana mtumishi anayelima shambani au anayechunga kondoo, je, mtumishi huyo arudipo atamwambia, ‘Karibu hapa keti ule chakula?’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ikiwa mmoja wenu ana mtumishi anayelima shambani au anayechunga kondoo, je, mtumishi huyo arudipo atamwambia, ‘Karibu hapa keti ule chakula?’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini, ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au achungaye ng'ombe, atakayemwambia mara arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule chakula?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Tuseme mmoja wenu ana mtumishi ambaye analima shambani au anachunga kondoo. Je, anaporudi kutoka shambani, atamwambia huyo mtumishi: ‘Haraka, njoo ule chakula?’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwenu yuko mwenye mtumwa wa kulima au wa kuchunga atakayemwambia huyo, akirudi toka shamba: Sasa hivi njoo, ukae chakulani?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini, ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au achungaye ng’ombe, atakayemwambia mara arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule chakula?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Tuseme kwa mufano, kati yenu kuna mutu mumoja anayekuwa na mutumishi anayemulimia au kumuchungia nyama wake. Mutumishi yule anaporudia toka kwenye shamba ataweza kumwambia kwamba aikae mara moja kula chakula?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini nani kwenu mwenye mtumishi anaelima, an anaeehunga kondoo? je! amwambia marra atakapoingia, akitoka mashamba, Njoo upesi, keti, ule chakula?